Saturday, 1 July 2017

ALIVYOAPISHWA RAIS WA CHUO KIKUU CHA AJUCO



RAIS WA AJUCO NA MAKAMU WAKE

Hatimaye ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ni leo tarehe 1/7/2017 katika ukumbi wa NYERERE 0NE ,ambapo rais aliyeshinda kiti cha urais katka chuo kikuu cha AJUCO  MR. SUNGURA ameapishwa , pamoja na makamu wake wa rais MADAM KOLADINA, na baada ya kuapishwa watakabidhiwas ofisi na kuanza kutekeleza majukumu yake ya kiuongozi.

SUNGURA

''Naahidi nitaimarisha elimu bora na itakuwa ni ya kibiashara, yenye manufaa kwa wanafunzi wa AJUCO.''

SUNGURA

''Nawaomba wanafunzi wenzangu kuwa linapotokea tatizo tufuate ngazi moja baada ya nyingine ktk kutatua matatizo yetu na siyo kuenda moja kwa moja kwa PRINCIPAL''.

SUNGURA

''Nimeamua/Niliamua kumchagua Madam KOLADINA ili aweze kutusaidia kutatua changamoto za kisheria ili kila mwanachuo ajue haki zake''

Thursday, 29 June 2017

SIKIA ALICHOKIONGEA RAIS MTEULE SUNGURA (AJUCSO )

Jana tarehe 28/6/2017 Chuo kikuu kishiriki cha AJUCO ambacho ni Tawi la SAUT ulifanyika uchaguzi wa kuwapata wabunge na Rais watakao hudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja. Wagombe wengi walijitokeza kuwania nafasi za ubunge lakini kwa upande wa Urais  hali ilikuwa ngumu sana kwani wagombea watatu wa kinyang'nyilo cha urais walipatikana watatu tu ambao ni Mr. January, Mr. Adam na Lomituni, ambao baada ya mchujo Mr. January na  Mr. Adam ndyo waliingia kwenye kinyang'anyilo hicho na hatimaye baada ya safari ndefu ya kampeni,na hatimaye kupiga kura Mr.Adam alpata kura 143 na Mr. Sungura alipata kura 522 na kutangazwa mshindi wa kiti cha urais. Wabunge walioshinda ni pamoja na WAILES TYSON First year 'A', MWANYIKA FELIX First year 'B' na CHUMA MATHIAS Second year.
SIKILIZA SAUTI YA RAISI MTEULE NA ALIYEKUWA MPINZANI WAKE HAPO CHINI
AU CLICK LINK HII>>>>>>>>https://www.youtube.com/watch?v=MwEoRioHIv4

Sunday, 25 June 2017

Mbwa mwenye sura mbaya zaidi duniani atajwa

Martha, ametajwa kuwa mbwa mwenye sura mbaya zaidi duniani.Haki miliki ya pichaEPA
Image captionMartha, ametajwa kuwa mbwa mwenye sura mbaya zaidi duniani.
Martha, ametajwa kuwa mbwa mwenye sura mbaya zaidi duniani.
Shindano la kila mwaka ambalo sasa liko katika mwaka wake wa 29 lilifanyika katika eneo la Petalum mjini Carlifornia.
Martha anayemilikiwa na Shirly Zindler aliwashinda wapinzani 13 na kupewa taji na pesa taslimu dola 1,500.
Mbwa huyo mwenye taya kubwa sasa atasafirishwa hadi mjini New York kwa maonyesho ya vyombo vya habari kulingana na waandalizi wa shindano hilo.
Maonyesho hayo ya Sonoma Marin yanasema kuwa shindano hilo huwashirikisha mbwa wengi ambao wameokolewa katika makaazi na maeneo ya kukuza mbwa kwa lengo la kuwauza.
Mbwa mwenye sura mbaya zaidi dunianiHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMbwa mwenye sura mbaya zaidi duniani
Martha ni mbwa aliyeokolewa ambaye karibia awe kipofu kutokana na kupuuziliwa mbali alisema bi Zindler.
''Baada ya kufanyiwa upasuaji sasa anaweza kuona tena na hahisi uchungu wowote''.
Shirika la habari la AP limesema kua Martha aliibuka mshindi kwa kutembea katika ukumbi na kuwavutia majaji.
Majaji hao walimpatia ushindi mbwa huyo kutokana na hisia za watu, sura, tabia na hisia zake.
source:bbc

Saturday, 24 June 2017

JIFUNZE HIKI: DOWNLOAD MOVIES NA MUSICS BURE YOUTUBE BILA KUWA NA DOWNLOADER YEYOTE

JINSI YA KUDOWNLOAD VIDEO  YEYOTE YOUTUBE BILA KUWA NA DOWNLOADER YEYEOTE

1) Go to www.youtube.com. Open the page of the video you want to download.


2) Add "ss" between the www. and the youtube.com section of the URL and hit enter. 


Example:


Original YouTube URL:  http://www.youtube.com/watch?v=ykF-rktutV4&list=CLTaJ1PHDR84I&feature=plcp


Modified YouTube URL: http://www.ssyoutube.com/watch?v=ykF-rktutV4&list=CLTaJ1PHDR84I&feature=plcp



3) This will redirect your browser to another site SaveFrom.net:


4) Choose the format of the video. Click on the link of the format. 
  
5) And your download will start in your downloader.



ENJOY YOUR TIME IN MUSICS AND MOVIES

Monday, 19 June 2017

Watu wenye silaha washambulia eneo la watalii Mali

Le Campement Kangaba, eneo lililoshambuliwaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionLe Campement Kangaba, eneo lililoshambuliwa
Vyombo vya Usalama nchini Mali vinasema vimeokoa zaidi ya wageni thelathini kutoka katika kituo kimoja cha Utalii, kilichokuwa kikishambuliwa na watu waliokuwa na silaha.
Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Salif Traore amethibitisha kuuawa kwa watu wawili, baada ya watu wanaohisiwa kuwa ni wapiganaji wenye itikadi kali kushambulia eneo hilo la starehe la Le Campement Kangaba lililoko nje ya mji mkuu wa nchi hiyo Bamako.
Kwa mujibu wa Waziri huyo wa Usalama, mmoja wa washambuliaji hao alifanikiwa kutoroka, baada ya kujeruhiwa, huku akiacha bunduki na chupa zilizokuwa na vifaa vya milipuko.
Aidha amesema watu wawili akiwemo raia mmoja pia walijeruhiwa.
Majeshi ya Mali na Ufaransa yalifika katika eneo la tukio.
Wanajeshi wa Ufaransa eneo la tukioHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWanajeshi wa Ufaransa eneo la tukio
Kituo hicho cha utalii ni maarufu nyakati za juma la wiki na kuwa kivutio kwa raia wa Mali wenye uwezo na wale wa kigeni wanaoishi Bamako.
Mapema mwezi huu, Ubalozi wa Marekani mjini Bamako ulionya uwezekano wa kutokea mashambulizi katika siku za baadaye katika majengo ya wanadiplomasia wa magharibi na maeneo mengine katika mji wa Bamako ambako raia wa nchi za magharibi wanapenda kwenda.
Wapiganaji wa Kiislamu wameendelea kufanya mashambulizi nchini Mali licha ya kupoteza maeneo yao wanayoyashikilia wakati wa uvamizi uliofanywa na majeshi ya muungano yaliyokuwa yakiongozwa na Ufaransa mwaka 2003.

Marekani yatoa majina ya wanajeshi waliouwawa baharini



The USS Fitzgerald, damaged by colliding with a Philippine-flagged merchant vessel, on 17 June 2017.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionAjali hiyo ilisababisha shimo kubwa kweny meli ya kijeshi
Marekani imetangaza majina ya wanajeshi wake 7 ambao waliuawa wakati meli yao iligongana na ile ya mizigo katika eneo la bahari ya Japan siku ya Jumamosi.
Wanjeshi hao walipatikana katika maneo yaliyokuwa yamefurika maji ndani ya meli hiyo ya kivita ya USS Fitzgerald.
Wanajeshi wengine watatu walijeruhiwa kwenye kisa hicho ambacho kilitokea karibu na mji wa bandari wa Yokosuka.
Meli hiyo kwa sasa imepelekwa huko YokosukaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMeli hiyo kwa sasa imepelekwa huko Yokosuka
Wengi wa wanajeshi walikuwa wamelala wakati meli hizo ziligongana. Marekani inasema kuwa inafanya uchunguzi.
Wanajeshi hao waliripotiwa kutoweka baada ya ajali hiyo.
Kamanda wa meli ya kijeshi Joseph P Aucoin aliwaambai waandishi wa habari kuwa ajali hiyo ilisababisha shimo kubwa kwenye meli ya kijeshi.
Wanajehsi hao saba ni pamoja na:
  • Dakota Kyle Rigsby, 19
  • Shingo Alexander Douglass, 25
  • Ngoc T Truong Huynh, 25
  • Noe Hernandez, 26
  • Carlos Victor Ganzon Sibayan, 23
  • Xavier Alec Martin, 24
  • Gary Leo Rehm Jr, 37
Map showing location of USS Fitzgerald crash - 17 June 2017
Image captionRamani inayoonyesha eneo la ajali

Marekani yashambulia na kuiangusha ndege ya jeshi la Syria

US F/A-18E Super HornetHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNdege sawa na hii yaA F/A-18E Super Hornet ya Syria ndiyo iliangushwa
Muungano unaoongozwa na Marekani nchini Syria umeangusha ndege ya jeshi la Syria katika mkoa wa Raqqa.
Jeshi la Syria lilisema kuwa ndege yake ya kijeshi ilikuwa katika harakati za kushambulia kundi la Islamic State wakati ilishambuliwa siku ya Jumapili.
Imesema kuwa kisa hicho kitakuwa cha athari katika vita dhdi ya ugaidi.
Marekani ilisema kuwa ilichukua hatua za kujilinda baada ya serikali ya Syria kuangusha mabomu karibu na wapiganaji wanaoungwa mkono na Marekani.
Kisa hicho kilitokea mji wa Ja'Din ambao unashikiliwa na vikosi vya Syrian Democratic Forces (SDF).
Wapiganaji wa SDF wanaoungwa mkono na muungano unaoongozwa na Marekani wamezingira ngome ya IS huko Raqqa.
Saa mbili kabla ya ndege hiyo kuangushwa, Marekani ilisema kuwa vikosi watiifu kwa raisi wa Syria Bashar al-Assad viliwashambulia wapiganaji wa SDF na kuwajeruhi kadha.
Mapema mwezi huu, Marekani iliangusha ndege isiyo na rubani ya seriikali ya Syria, baada ya ndege hiyo kushambulia vikosi karibu na kivuko cha mpaka cha al-Tanf kwenye mpaka kati ya Syria na Iraq.

Tambua Madhara ya Ulaji wa Chipsi

Chips ni aina ya chakula ambacho hupendwa na watu wengi na pia ni miongoni mwa vyakula vyenye mafuta mengi. chips pia inasemekana ni miongoini mwa vyakula ambavyo hupikwa katika joto la juu zaidi ya 300 degree.

Chips ni chakula chenye mafuta mengi na mafuta yanapoingia mwilini huenda kuzunguka sehemu ya mwili wa mwanadamu. kama ni mtu ambaye mazoezi pia hufanyi madhara yake ni kupata magonjwa ya moyo. hivi sasa idadi kubwa ya vijana wanaugua magonjwa mengi yanayo sababishwa na mkusanyiko wa mafuta katika miili yao amabayo huchangiwa na kuto kufanya mazoezi madhara yake mafuta kuziba mirija

Mafuta yakiliwa sana husababisha kuzidi mwilini.
Pia inasadikika mafuta yaliyopo katika chipsi katika sahani moja ya chisi ya moto endapo utaamua kuchuja kuna uwezekano wa kupata nusu glasi ya mafuta ya kupikia. Kwa hali hii ujue ni hatari.

Na mwili huwa hatupi kinachofaa, na badala yake kama hakitumiki wakati huo basi huhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye. Ndio maana tunapokula vyakula vyingi vyenye mafuta mengi hutupelekea kuongeza unene na uzito.

Unene huwa ni chanzo cha magonjwa mengi ,Kwani (High Blood pressure) hutokana na kuwa na mafuta mengi mwilini ambayo hupelekea mirija ya kusafirisha damu kuwa na mafuta. Hii husababisha njia ya kupitia damu kuwa nyembamba hivyo kusababisha nguvu ya ziada itumike kusukuma damu hiyo ili isambae mwilini kama inavyotakiwa. Nguvu hii ya ziada huongeza au kupunguza mapigo ya moyo.

Mapigo ya moyo yanapoongezeka sana ni hatari na yanapo pungua sana pia ni hatari.
Hivyo basi ni vizuri kwa watumiaji wa chipsi kujitahidi kutumia kwa kiasi kidogo au kuacha kabisa vile vile mazoezi pia ni muhimu ili kupunguza mrundikano wa mafuta katika mwili.

Pia inasemekana kuwa wanasayansi wamegundua kuwa chipsi husababisha kukuza hips hivyo kwa wanaume wengi hawatapenda kuwa katika hali hiyo, hivyo ni muhimu kujiepusha na pia isije ikawa kichocheo kwa wanawake kutumia sana ili kukuza sehemu hizo za maumbile bali wapunguze kutumia chipsi pamoja na kufanya mazoezi ili kuweka mwili katika hali ya kuepuka magonjwa yasiyo ya lazima.pia ulaji wa chips kupita kiasi husababisha wanaume na wanawake kuzeeka mapema.

Mwanajeshi wa Korea Kaskazini ahamia K. Kusini kwa kuogelea

Mwanajeshi mmoja wa Korea Kaskazini ametorokea Korea Kusini kupitia kuvuka mto Han kwa kuogelea ,ikiwa ni mara ya pili kwa raia wa taifa hilo kuhamia kwa majirani zao.

Mkuu wa Jeshi nchini Korea Kusini amesema kuwa mwanajeshi huyo aliogelea na kupitia eneo moja jembamba sana la maji ya mto huo yalio na kasi kubwa baada ya kuvalia boya lilolomsaidia kuelea.
Wiki iliopita mwanajeshi mwengine wa Korea Kaskazini alipitia mpaka unaolindwa sana unaogawanya mataifa hayo mawili.

Wanajeshi walikuwa wakihamia Korea Kusini katika kiwango cha mmoja kwa mwaka.

Mwanajeshi huyo aliyedaiwa kuwa na miaka ya ishirini alipatikana katika eneo la Gimpo, Magharibi mwa mji mkuu wa Korea Kusini Seoul, kulingana na chombo cha habari cha Yonhap.

Alipiga kelele akisema ''musiniue'', niko hapa kuhama ,kwa mwanajeshi wa Korea Kusini ambaye alikuwa amemuona, kilisema chombo cha habari cha Yonhap.

Mwanajeshi huyo sasa atahojiwa na maafisa wa kijeshi, Korea Kaskazini na Kusini ziko katika vita baradi tangu mzozo kati yao umalizike 1953 kupitia makubaliano.

Seoul inasema kuwa zaidi ya raia 30,000 wa Korea Kaskazini wamehamia kusini tangu kumalizika kwa vita vya Korea, wengi wao kupitia China ambayo ina mpaka mrefu na Korea Kaskazini.


Ajinyonga kisa ugumu wa maisha

Kijana Paulo Ezekiel, amejinyonga kutokana na kile kinachodaiwa ugumu wa maisha.

Paulo (17) alikuwa anaishi na wazazi wake Mtaa wa Mazinge Kata ya Ndembezi mjini Shinyanga, alifariki dunia juzi usiku kutokana na kudaiwa kujinyonga kwa kamba juu ya mti jirani na nyumbani kwao.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi alfajiri baada ya marehemu kutoka nje ya geti la nyumba yao na kuelekea kwenye mti huo kisha kijipiga kitanzi kunakodaiwa kusababisha kifo chake.

Akizungumza tukio hilo jana, baba mzazi wa marehemu, Ezekiel alisema awali kijana wake alikuwa na ugomvi na marafiki zake ambao ni madereva bodaboda, lakini huo ulisuluhishwa na akaendelea na majukumu yake.

Alisema chanzo cha kifo chake hakijafahamika vizuri, lakini mara kwa mara alikuwa akilalamika kuwa maisha ni magumu.

"Ilipofika majira ya saa 10 usiku nilisikia mlango wa chumba cha kijana wangu ukifunguliwa, nikajua ametoka kwenda kujisaidia lakini muda mrefu ulipopita bila kusikia amerudi, ndipo nikatoka nje na kukuta geti la uani likiwa wazi, nikaanza kumtafuta bila mafanikio", alisema.

Aliongeza:
"Niliporudi ndani nikamwamsha mama yake mzazi na wadogo zake wa kike, tukaanza kumsaka ndipo tukamuona akiwa juu ya mti jirani na nyumba yetu, akiwa ameshafariki kwa kujinyonga na kamba".

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Jumanne Murilo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa na jeshi la hilo kuhusiana na tukio hilo.

Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga na unatarajiwa kuzikwa leo kwenye Makaburi ya Mtaa wa Dodoma mjini hapa.

Chanzo: Nipashe