Mwanajeshi mmoja wa Korea Kaskazini ametorokea Korea Kusini kupitia kuvuka mto Han kwa kuogelea ,ikiwa ni mara ya pili kwa raia wa taifa hilo kuhamia kwa majirani zao.
Mkuu wa Jeshi nchini Korea Kusini amesema kuwa mwanajeshi huyo aliogelea na kupitia eneo moja jembamba sana la maji ya mto huo yalio na kasi kubwa baada ya kuvalia boya lilolomsaidia kuelea.
Wiki iliopita mwanajeshi mwengine wa Korea Kaskazini alipitia mpaka unaolindwa sana unaogawanya mataifa hayo mawili.
Wanajeshi walikuwa wakihamia Korea Kusini katika kiwango cha mmoja kwa mwaka.
Mwanajeshi huyo aliyedaiwa kuwa na miaka ya ishirini alipatikana katika eneo la Gimpo, Magharibi mwa mji mkuu wa Korea Kusini Seoul, kulingana na chombo cha habari cha Yonhap.
Alipiga kelele akisema ''musiniue'', niko hapa kuhama ,kwa mwanajeshi wa Korea Kusini ambaye alikuwa amemuona, kilisema chombo cha habari cha Yonhap.
Mwanajeshi huyo sasa atahojiwa na maafisa wa kijeshi, Korea Kaskazini na Kusini ziko katika vita baradi tangu mzozo kati yao umalizike 1953 kupitia makubaliano.
Seoul inasema kuwa zaidi ya raia 30,000 wa Korea Kaskazini wamehamia kusini tangu kumalizika kwa vita vya Korea, wengi wao kupitia China ambayo ina mpaka mrefu na Korea Kaskazini.
Monday, 19 June 2017
Home »
» Mwanajeshi wa Korea Kaskazini ahamia K. Kusini kwa kuogelea
0 comments:
Post a Comment