Saturday, 17 June 2017
Home »
» Hii Ndio Sababu ya Cristiano Ronaldo kutaka kufunga virago Madrid
Hii Ndio Sababu ya Cristiano Ronaldo kutaka kufunga virago Madrid
MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo ameamua kuondoka Real Madrid baada ya kuwaambia wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Ureno nia yake, kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania.
Mustakabali wa Ronaldo Real Madrid haueleweki kutokana na mshambuliaji huyo kusema hana furaha kufuatia kesi ya kukwepa kodi Hispania, Pauni Miklioni 13. Ameionya klabu hiyo ataondoka iwapo atatiwa hatiani.
Na gazeti la la Marca la mjini Madrid limesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 atafanya hivyo baada ya kuwaeleza wachezaji wenzake wa timu ya taifa mipango yake.
Ronaldo kwa sasa yuko Urusi na kikosi cha Ureno kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mabara Confederations kujaribu kurudia mafanikio yao ya Euro 2016 nchini Ufaransa.
Nukuu katika gazeti la Marca inasema kwamba Ronaldo amewaambia wachezaji wenzake: "Ninaondoka Real Madrid. Nimefanya maamuzi. Hakuna kurudi nyuma.'
Paris Saint-Germain ikitajwa kama klabu ya kwanza ambayo mchezaji huyo anaweza kujiunga nayo, inatarajiwa kuanza rasmi kuifukuzia saini ya Cristiano Ronaldo kama mshindi huyo wa Ballon d'Or nne ataondoka Real baada ya msimu mzuri akiiachia taji la La Liga na Ligi ya Mabingwa.
Manchester United ingependa kumrejesha nyota huyo Mreno huyo Old Trafford, lakini kwanza wanatakiwa kuchunguza baada ya taarifa ya kufanyika kikao cha siri kati ya wakala wa Ronaldo, Jorge Mendes na Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi mjini Cardiff mchana kabla ya fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Inafahamika Mendes amemuambia Al-Khelaifi juu ya matatizo hayo yanavyozidi kukuwa na amemuahidi kuendeleakuwasiliana kupeana taarifa zaidi.
PSG imekuwa ikimfukuzia mwenye umri wa miaka 32 kwa miaka sasa itakuwa tayari kutumia kiasi chochote cha fedha ili kumpata Ronaldo.
Related Posts:
Mashabiki wa kandanda 1000 wajeruhiwa kwenye mkanyagano ItaliaHaki miliki ya pichaEPAImage captionMashabiki wa kandanda 1000 wajeruhiwa kwenye mkanyagano Italia Takriban watu 1000 wamejeruhiwa katika mji wa Turin nchini Italia baada ya fataki kuzua hofu na kusababisha mkanyagano usiku w… Read More
Hii ndio idadi ya watu wanaosafiri kwenye mabasi ya mwendokasi kwa siku Dar es Salaam. Mradi wa mabasi yaendayo haraka (BRT) sasa unasafirisha watu 200,000 kwa siku kutoka watu 50,000 iliyokuwa ikisafirisha mwaka jana baada ya mradi huo kuanza kazi.Kuongezeka kwa idadi hiyo inaelezwa kuwa ni is… Read More
Lowassa amponza Yericko Nyerere Mfuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendele (Chadema) Yericko Nyerere amepandishwa Kizimbani na kusomewa mashtaka Matano yanayohusu kusambaza Taarifa za Uoungo kupita mtrandoa wa Facebook.Mbele ya Hakimu Mkazi Wilbard Mashua… Read More
Serikali yazuia nyasi bandia za Simba Hii ni nyingine mpya kuwa, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambalo ni taasisi ya serikali, limezuia nyasi bandia za Klabu ya Simba zilizopo kwenye bandari ya Dar es Salaam.Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu Simb… Read More
Marekani yaionya China kuhusu visiwa bandia bahariniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionChina ni moja ya nchi zinazodai kumiliki maeneo ya kusini mwa bahari ya China Marekanai hautakubali China kuweka wanajeshi kwenye visiwa ilivyojenga Kusini mwa bahari ya China, waz… Read More
0 comments:
Post a Comment