Kegera Sugar hawaelewi lolote kuhusiana na mshambuliaji Mbaraka Yusuf, wanasema ni mali yao.
Msisitizo wa Kegera Sugar wanasema wanataka walipwe shilingi milioni 150 ili imuachie mshambuliaji huyo kwenda Azam FC ambako tayari amesaini.
Hatua hiyo imekuja siku chache tangu Meneja wa Kagera, Mohammed Hussein kupiga hodi kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), akidai mshambuliaji huyo amesajiliwa kimakosa.
Mbaraka alisaini mkataba wa kuichezea Azam hivi karibuni kwa dau la zaidi ya shilingi milioni 40 akiwa kwenye kambi ya Taifa Stars.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Ijumaa limezipata kutoka ndani ya uongozi wa Kagera, mshambuliaji huyo aliingia makubaliano ya kusaini mkataba wa miaka miwili akiwa bado amebakiza mwaka mmoja.
Mtoa taarifa huyo alisema uongozi wa Kagera umekubali kumuachia mshambuliaji huyo kwa makubaliano ya kulipwa shilingi milioni 150 ambazo wanazihitaji wao.
Aliongeza kuwa, kama Azam hawatakubali kutoa fedha hizo, basi suala hilo litafika mbali ikiwemo Fifa kutokana na timu hiyo kumsainisha mchezaji akiwa ana mkataba bado wa miaka miwili.
Alipotafutwa Meneja wa Kagera, Mohammed Hussein kuzungumzia hilo, alikiri mchezaji huyo kuwa na mkataba na Kagera na kusema wameshapeleka malalamiko yao kwa TFF juu ya kitendo hicho.
SOURCE: CHAMPIONI
Friday, 16 June 2017
Home »
» Kagera Sugar yaibua mapya kuhusu mshambuliaji Mbaraka Yusuf
0 comments:
Post a Comment