Saturday, 17 June 2017

Takukuru: Tunaendelea Kuwahoji watuhumiwa wa Makinikia

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru imesema kuwa inaendelea kuwahoji watuhumiwa wote walitajwa kwenye sakata la kusafirisha Makinikia ya madini nje ya nchi

Ofisa Habari wa  (Takukuru), Mussa Misalaba, amesema kuwa taasisi yao inaendelea na uchunguzi kufuatilia endapo kuna vitendo vya rushwa kwa wote waliohusika na masuala ya usafirishaji wa makinikia.

“Sisi tunaangalia rushwa iliyopo kwenye hiyo biashara kwa kuwa pale kuna wadau wengi… kuna wengine hawahusiki kwenye mikataba na wengine wapo kwenye utekelezaji. Siwezi kusema ni wangapi tumewahoji ama ambao wanatarajiwa kuhojiwa. Kazi yetu inaendelea,” alisema Misalaba.

0 comments:

Post a Comment