Wednesday 14 June 2017

SOMA: Ronaldo alivyojitetea kuhusu tuhuma za ukwepaji kodi

Mchezaji huyo, jana Jumanne aliandikiwa barua na akitakiwa kujibu mashtaka yaliyoandaliwa na mamlaka ya kodi mjini Pozuelo de Alorcon.
Mwanasheria wa Cristiano Ronaldo amepinga vikali tuhuma zinazoelekezwa kwa mshambuliaji huyo wa Real Madrid kuhusu kujipatia fedha nyingi bila kulipa kodi kwenye mamlaka husika nchini Hispania.

Mchezaji huyo, jana Jumanne aliandikiwa barua na akitakiwa kujibu mashtaka yaliyoandaliwa na mamlaka ya kodi mjini Pozuelo de Alorcon.

Mwanasheria huyo alisema hiyo ni mbinu ya kumchafua mshindi huyo wa Tuzo ya Ballon d’Or huku akisema amekuwa akitimiza wajibu wake kwa kulipa kodi kwa hiari.

Mashtaka yaliyoandaliwa kwake, inadai wa kwamba Ronaldo amekuwa akijitengeneza fedha nyingi tangu kupitia matangazo ya picha zake kuanzia mwaka 2011 na 2014.

Taarifa iliyotolewa na mwanasheria huyo inaeleza kwamba Ronaldo amekuwa akishirikiana vyema na mamlaka za kodi. Hata hivyo kiasi kilichotajwa wakae chini kujadiliana, lakini hakuna njama zozote kwa mchezaji huyo kukwepa kodi.

0 comments:

Post a Comment