Monday, 19 June 2017

Ole Sendeka atuma salamu hizi kwa Lowassa

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amempongeza Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa kumpongeza Rais John Magufuli kufuatia uamuzi aliouchukua kuhusu mchanga wa madini yanayochimbwa nchini na kampuni ya Acacia.

Ole Sendeka ambaye aliwahi kuwa msemaji wa Chama Cha Mapinduzi, amesema kuwa baada ya kusikia kupitia vyombo vya habari kuwa Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema amempongeza Rais, hana budi kumshukuru na kumpongeza pia kwa kufanya hivyo, na kuwaomba wabunge wote bila kujali vyama vyao kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kusimamia kikamilifu rasilimali za nchi.

“Nanyi wabunge mkiwa bungeni muungeni mkono Rais wetu Magufuli anavyotetea rasilimali za nchi ili madini yanayochimbwa yaweze kuwanufaisha Watanzania, waweze kupata huduma zao za msingi kupitia madini hayo,” Ole Sendeka anakaririwa na Mwananchi.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Njombe alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza jana kwenye mazishi ya mama yake mzazi yaliyofanyika katika kijiji cha Losokonoi wilayani Simanjiro.

 Alimuomba mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya ambaye alihudhuria mazishi hayo, kumfikishia salamu na pongezi hizo kwa Lowassa.

Lowassa alimpongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wake baada ya kupokea ripoti ya pili ya uchunguzi wa makontena ya mchanga wa madini yanayoshikiliwa na Serikali katika bandari ya Dar es Salaam, yalipokuwa katika mchakato wa kusafirishwa nje ya nchi na kampuni ya Acacia.

Related Posts:

  • Wakamatwa na dawa za kulevya Mwanza Jeshi la Polisi Mwanza linawashikilia watu wanne baada ya kuwakuta na dawa za kulevya aina ya Mirungi mafungu 57 yenye ukubwa wa kilogramu 56.75 ambayo yalikuwa yamewekwa kwenye mabegi na magunia.Kamanda wa Polisi Mwanza, A… Read More
  • Ester Bulaya asema: Hamjatuziba midomo Mbunge wa Bunda Mjini Mh. Ester Bulaya ametoa salamu kwa Wabunge wa CCM pamoja na Spika Job Ndugai kutambua kwamba hata baada ya kumuadhibu kutohudhuria vikao bya bunge siyo silaha ya kuwafunga midomo.Bulaya amefunguka hayo… Read More
  • Diamond Platnumz ataja moja ya vigezo vya kujiunga na familia ya WCB Mwimbaji staa wa Bongofleva kutoka WCB Diamond Platnumz amefunguka kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM na kusema kuwa sifa ya kwanza ya WCB ni kumtoa msanii kwenye hali ngumu ili waweze kufanikiwa wote kwa kuwa huwa na adabu na… Read More
  • Mwanasheria Mkuu wa TBS Afikishwa Mahakamani Mwanasheria Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Baptister Marco (54) amepandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu ya kuishi na kufanya kazi nchini bila kuwa na  kibali.Mwendesha Mashtaka w… Read More
  • Gerard Pique awaponda tena Real Madrid. Kama kuna kitu kinawakera mashabiki wa Real Madrid baasi ni mtu anayeitwa Gerard Pique, mlinzi huyu wa kati wa Barcelona amekuwa hawezi kuikalia kimya Real Madrid hata kama wamefungwa au wameshinda.Baada ya Real Madrid kufa… Read More

0 comments:

Post a Comment