MKALI wa Ngoma ya Hela, Hamad Ally ‘Madee’ amewashangaa baadhi ya mastaa ambao katika Mwezi wa Mfungo wa Ramadhani wamekuwa na utamaduni wa kutoa vitu kwa jamii na kupiga picha kisha kujionesha kwenye mitandao ya kijamii kitu ambacho siyo sawa na matakwa ya Dini ya Kiislamu.
Akipiga stori na Show Biz, Madee alisema, kwa upande wake suala la kujitoa kwa jamii inayomzunguka ndiyo limemfi kisha katika mafanikio hayo aliyonayo na kuwa hufanya hivyo mara kwa mara na hata pale anapofanya hawezi kujinadi kwenye mitandao ya kijamii kama baadhi ya wasanii wanavyofanya.
“Unajua katika Dini ya Kiislamu hatujaelezwa kutoa na kujinadi kwenye mitandao ya kijamii.
Tumetakiwa kutoa kwa moyo. Sasa kwa upande wangu huwa ninawashangaa sana baadhi ya mastaa ambao wakitoa misaada basi kwao hiyo ndiyo inakuwa kiki.
“Kiukweli si sawa na wanatakiwa kubadilika maana huko mitaani kuna watu wengi mno wanatoa lakini hawajitangazi kama wao,” alimaliza Madee.
0 comments:
Post a Comment