Thursday 8 June 2017

Aliyeuwa na kujificha miaka 45 akamatwa Japan



Idara ya polisi inasema kuwa imethibitisha kuwa kwa hakika ni mtoro Bw. Osaka, baada ya kuchunguza chembechembe za damu yake-DNAHaki miliki ya pichaAFP
Image captionIdara ya polisi inasema kuwa imethibitisha kuwa kwa hakika ni mtoro Bw. Osaka, baada ya kuchunguza chembechembe za damu yake-DNA
Kisa cha mshukiwa mmoja wa mauwaji nchini Japan, kimethibitisha kuwa, unaweza kukimbia kwa miaka mingi, lakini hutaweza kujificha daima, kwani siku moja utakamatwa.
Mwanamapinduzi wa mrengo wa kushoto Masaaki Osaka, amekamatwa na kuhukumiwa kwa kosa la kumuuwa afisa mmoja wa polisi, wakati wa maandamano yaliyofanyika katika barabara za mji mkuu Tokyo, miaka 45 iliyopita.
Anadaiwa alimchoma moto afisa huyo kwa bomu la petroli la kujiundia maarufu kwa jina Molotov Cocktail petrol bomb.
Hakuna mshukiwa wa uhalifu amewahi ambaye amehepa vyombo vya usalama kwa muda mrefu kiasi hicho, vyombo vya habari nchini Japan vimeripoti.
Serikali ya Japan haina hukumu ya kifo.
Kifungo kirefu cha miaka 15, kilifutiliwa mbali mwaka 2010.
Masaaki Osaka amekuwa akisakwa na polisi tangu mapema miaka ya 1970sHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMasaaki Osaka amekuwa akisakwa na polisi tangu mapema miaka ya 1970s
Ni wapi wanaotoroka kutoka magerezani na vifungoni hukimbilia?
Bwana Osaka alikamatwa mwezi uliopita ndani ya nyumba moja mjini Hiroshima inayomilikiwa na Chukaku-ha, au makao ya vuguvugu la Revolutionary Communist League (JRCL).
Tangu alipokamatwa, maafisa wa polisi wanasemekana walimtaka anyamaze kimya.
Awali mtoro huyo alituhumiwa kwa kosa la kuzuia polisi kufanya kazi yao- kabla ya polisi kung`amua alikuwa nani.
Mnano Jumatano wiki hii, alihamishiwa Tokyo kutoka Hiroshima, ili kuhojiwa zaidi, hayo ni kwa mjibu wa taarifa za vyombo vya habari nchini Japan.
Polisi inasema kwamba, imemtambua kupitia uchunguzi wa DNA uliofanywa, kwa sababu alama ya vidole havikupatikana wakati alipotekeleza uhalifu.
Picha ya Mtoro Osaka ya kukamatwa kwake ilisambazwa kila mahali nchini Japan kwa miongo minneHaki miliki ya pichaEPA
Image captionPicha ya Mtoro Osaka ya kukamatwa kwake ilisambazwa kila mahali nchini Japan kwa miongo minne
Wanasema kuwa Bw. Osaka aliweza kufaulu kukwepa mkono mrefu wa sheria kwa miaka mingi kiasi hicho, kwa sababu ni mmojawepo wa wanachama wa ngazi za juu wa vuguvugu hilo la mrengo wa kushoto la JRCL na alisaidiwa na washirika wake.
Vuguvugu la JRCL, lilianzishwa miaka ya 1950s na miaka ya 1960s na 1970s lilifahamika kwa kupanga maandamano mabaya yenye ghasia.
Bw. Osaka anatuhumiwa kwa kumuuwa afisa mmoja wa polisi mwenye umri wa miaka 21wakati wa ghasia mbaya katika kata ya Shibuya, Jijini Japan mnamo mwaka 1971.
Inasemekana alimgonga kwa fimbo ya chuma kabla ya kumteketeza.
Vuguvugu la JRCL linapinga vitu vingi, vikiwemo hatua ya Marekani kujaza wanajeshi wake Japan.
Matukio makubwa yaliyotokea nchini Japan muda wote Masaaki Osaka alikuwa mbioni:
1972 - Waziri mkuu wa Japan azuru China na uhusiano wa kidiplomasia ukarejeshwa.
1993 - Serikali ikatoa taarifa ya kihistoria maarufu "Kono statement" ikiomba msamaha kwa niaba ya wanajeshi wake wakati wa vita kuu kuwatumia wanawake kama wafungwa wa ngono.
1995 - Tetemeko la ardhi lagonga katikati mwa Japan, huku maelfu wakiuwawa.
2011 Februari- China ikaipiku Japan kama taifa la pili kwa uchumi mkubwa duniani.
2011 Machi - Tetemeko kubwa lakumba ufukwe wa Japan na kusababisha kabobo la Tsunami, huku maeneo mengi yakiathirika vikiwemo vinu vya kinuklea vya Fukushima na kusababisha kuvuja kwa miale.
2014 - Serikali ya Japan,yaidhinisha mabadiliko makubwa katika idara yake ya jeshi, na kuanzisha fursa ya majeshi yake kutumika katika ujumbe wa kupigana nje ya nchi.

0 comments:

Post a Comment