Monday, 5 June 2017

Mbasha ahofia kupata shambulio la moyo.

MWIM-BAJI wa Mu-ziki wa Injili, Emmanuel Mbasha ameibuka na kusema kuwa amekubaliana na yote kwa aliyekuwa mkewe, Flora Mbasha ili kuepuka yaliyompata mzazi mwenzake na Zari, Ivan Ssemwanga wa Uganda ya kufariki dunia kwa shambulio la moyo.

Akipiga stori na Over Ze Weekend baada ya habari kuzagaa kwamba ana msongo wa mawazo unaosababishwa na aliyekuwa mkewe, Flora ambaye kwa sasa ni mke wa mtu, alikanusha vikali akisema yupo sawa na hawezi kuwa hivyo kwa kuwa amekubaliana na kila kilichotokea.

“Sitaki kupata tatizo la moyo na tangu mwanzo hata kabla hatujaachana kwa talaka mahakamani mawazo mabaya yalikuwa yakinijia nikayakataa kwa sababu ningeyasikiliza ningejikuta nikiziharibu ndoto zote za maisha yangu, nilishayakubali yote, nimeshazoea hiyo hali” alisema Mbasha.

Aliendelea kueleza kuwa sababu za kumweka Flora kwenye ukurasa wake wa Instagram siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake aliyokuwa akiadhimisha Juni Mosi, mwaka huu na kumtakia mema ni kutokana na upendo tu kwani siku hiyo huwa inamkumbusha mengi waliyokuwa wakiyafanya.

“Nakumbuka kila tarehe moja ya mwezi wa sita kila mwaka tulivyokuwa tunaifurahia, namnunulia zawadi tunafanya pati kidogo nyumbani au sehemu yoyote,.

“Kuposti kwangu huko nimeshangaa watu maneno yamewatoka sana kwa kweli, niliposti kiroho safi tu na kwa upendo maana nilishayakubali matokeo, sina msongo wa mawazo maana najua ni hatari naweza nikapoteza uhai kama ilivyotokea kwa mume wa Zari, Ivan nikashindwa kutimiza ndoto zangu za kuwa mfanyabiashara mkubwa na mtumishi wa Mungu mku-bwa sana duniani,” alisema.

source:muungwana

0 comments:

Post a Comment