Friday, 16 June 2017

Kauli ya Zitto Kabwe kufuatia kufungiwa kwa Gazeti la Mawio

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto kabwe amepinga vikali hatua ya kufungiwa kwa gazeti la MAWIO na kudai kuwa hatua hiyo inawanyima Wananchi mawazo mbadala.
==>Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Zitto ameandika yafuatayo;
“Uamuzi wa kufungia gazeti la Mawio unapaswa kulaaniwa na kila mwanademokrasia. Uhusika wa Marais wastaafu kwenye mikataba ya madini umesemwa na Rais Magufuli Mwenyewe sio Mawio.
"Hakuna mkataba ulioingiwa bila Baraza la Mawaziri kuidhinisha. Kitendo cha Kamati ya Rais kutuhumu Mawaziri wa zamani mbele ya Rais Magufuli na yeye Mwenyewe Rais Magufuli kusema hatapona mtu ilikuwa ni dhahiri kuwa Rais anawachimba watangulizi wake.
"Kwa sisi tuliofundishwa lugha ya Uongozi tuling’amua mapema kuwa Rais Magufuli alikuwa anawatuhumu wenzake. Hivyo Gazeti la Mawio lilitafsiri tu maelezo ya Rais. Kitendo cha Rais kuonya kuwa Marais wastaafu waachwe ilikuwa ni KUJISEMESHA tu na kufungia gazeti la Mawio ni ‘ panick ‘ ya Rais Magufuli baada ya kuwasema watangulizi wake.
"Kila wakati Rais analia kuhujumiwa na kutaka kuombewa; Adui wa Magufuli ni Magufuli mwenyewe.
"Serikali ifungulie Gazeti la Mawio mara moja bila masharti kwani kulifungia ni kuwanyima Watanzania mawazo mbadala kuhusu mambo ya hovyo yanayoendelea nchini kwetu.
na kumalizia kwa hashtag ya #PressFreedom #UhuruWaHabari.”

Related Posts:

  • Mauaji Pwani yamepangwa: Mbunge Dodoma. Mauaji katika wilaya za Kibiti na Rufiji jana yaliibuka bungeni kwa mara ya pili, wakati mbunge wa Rufiji (CCM), Mohamed Mchengerwa alipoeleza siri ya mipango na kiini chake.“Nataka niseme na Rais wangu ajue. Mambo … Read More
  • Kashfa nzito zaikumba Wizara ya maliasili BAADHI ya wabunge wamelalamikia vitendo vinavyofanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii, kukamata na kupiga mnada mifugo inayoingia kwenye hifadhi za taifa. Kutokana na vitendo hivyo, watunga sheria hao wameishauri serik… Read More
  • Msanii aliyebuni nembo ya Taifa sakata lake latua bungeni Dodoma. Bunge jana lilielezwa kuwa msanii aliyebuni na kutengeneza nembo ya taifa ya Bibi na Bwana, Francis Ngosha ametelekezwa na taifa na anaishi maisha magumu.Suala la msanii huyo liliibuka Bungeni mjini Dodoma leo, kuto… Read More
  • Jackline Wolper: Diamond ni zaidi ya mpenzi wangu Jackline Wolper Muigizaji Jackline Wolper amesema yeye na msanii Diamond Platnumz wana uhusiano wao ambao ni kiwango cha juu kwani wamekuwa wakishirikiana katika mambo mengi.Katika segment ya kikaongoni inayorushwa na EA… Read More
  • Kikwete aanza kazi na Mgogoro wa Libya Rais Mstaafu Jakaya Mrisho kikwete ameanza kazi kama Mwenyekiti Mwenza katika Baraza la Kimatifa la Wakimbizi ambapo ameanza kazi yeye na jopo lake ya kutaka kusuluhisha Mgororo wa muda mrefu wa nchin ya Libya. Kikwete … Read More

0 comments:

Post a Comment