Tuesday, 13 June 2017

Korea Kaskazini yamwachilia huru Mmarekani

Otto Frederick Warmbier, flanked by two North Korean guardsHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWazazi wa Otto Warmbier waliohifia usalama wa mwana wao kufuatia kuongezeka kwa uhsama kati ya Marekani na Korea Kaskazini
Korea Kaskazini imemwachilia huru mwanafunzi Mmarekani Otto Warmbier ambaye alikuwa amefungwa jela katika taifa hilo la bara Asia, waziri wa mambo ya nje wa Marekani amesema.
Bw Warmbier, 22, alihukumiwa kufungwa jela miaka 15 na kazi ngumu Machi 2016 baada ya kupatikana na hatia ya kujaribu kuiba bango la propaganda kutoka kwenye hoteli moja.
Bw Tillerson amesema Bw Warmbier sasa yuko njiani kurejea Marekani ambapo ataungana tena na jamaa zake Cincinnati, Ohio.
Gazeti la Washington Post limemnukuu babake Fred akisema mwanawe wa kiume amesafirishwa kama mgonjwa wka sababu hana fahamu.
Gazeti hilo linasema wazazi wa Warmbier waliambiwa mwana wao wa kiume alianza kuugua ugonjwa wa botulism, ugonjwa nadra ambao humfanya mtu kupooza, muda mfupi baada ya kesi yake kumalizika miezi 15 iliyopita.
Alipewa dawa za kumfanya alale, na tangu wakati huo hajawahi kupata fahamu tena.
"Mwana wetu anarejea nyumbani," Fred Warmbier amenukuliwa akisema.
"Kwa sasa, tunachukulia hiki kuwa kisa cha ajali tu. Tutamuona tena mwana wetu Otto leo usiku."

Alilazimishwa kukiri mashtaka?

Otto Warmbier, mwanafunzi aliyekuwa amehitimu na shahada ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Virginia, alikuwa amezuru Korea Kaskazini kama mtalii akiwa na shirika la Young Pioneer Tours alipokamatwa 2 Januari 2016.
Alitoa hotuba kwenye televisheni akikiri mashtaka mwezi mmoja baadaye, ambapo alisema kwamba alikuwa amekusudia kubeba bango hilo kama "kumbukumbu" kwa kanisa moja la Marekani.
Aliongeza kuwa "lengo langu lilikuwa kudhuru moyo na kujitolea kwa watu wa Korea kufanya kazi.
Haijabainika iwapo alitoa hotuba hiyo kwa hiari au alilazimishwa.
Hata hivyo, wafungwa kutoka nchi za nje nchini Korea Kaskazini wamekuwa mara kwa mara wakikana taarifa walizozitoa wakikiri makosa, wakisema kwamba walishinikizwa kutoa hotuba hizo.
Baada ya kesi iliyodumu mdua mfupi 16 Machi, Bw Warmbieri alihukumiwa kufungwa jela miaka 15 na kufanyishwa kazi ngumu.
Wazazi wake Fred na Cindy waliambia CNN mapema mwezi huu kwamba walikuwa hawajawasiliana na mwana wao kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Walieleza wasiwasi wao kuhusu hatima yake hasa baada ya uhasama kati ya Korea Kaskazini na Marekani kuzidi kutokana an hatua ya Pyongyang kufanyia majaribio makombora ya masafa marefu.
Meli za kivita za Marekani zilitumwa eneo hilo.
Rodman atua Pyongyang
Bw Warmbier ameachiliwa saa chache baada ya nyota wa mpira wa kikapu wa Marekani Dennis Rodman kutua Korea Kaskazini.
Haijabainika iwapo matukio hayo mawili yana uhusiano wowote.
Bw Rodman ni rafiki wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un na amezuru nchi hiyo mara kadha miaka ya karibuni.
Dennis Rodman mobbed by the press en route to PyongyangHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionDennis Rodman aliandamwa sana na wanahabari uwanja wa ndege Beijing akielekea Pyongyang
Alisema amezuru taifa hilo kama raia binafsi, na "lengo langu ni kuona iwapo ninaweza kuleta michezo hapa Korea Kaskazini".
Raia wengine watatu wa Marekani bado wanazuiliwa Korea Kaskazini.
Kim Dong-chul, 62, mmishenari wa Marekani mwenye asili ya Korea, Profesa Mmarekani mwenye asili ya Korea Kim Sang-duk (auTony Kim); naKim Hak-song, aliyekuwa akifanya akzi Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Pyongyang (PUST).

Related Posts:

  • Mbunifu wa Android azindua simu mpya ya EssentialHaki miliki ya pichaESSENTIAL PHONEImage captionSinu ya Essential hutumia mfumo wa Android na imeanza kuuzwa nchini Marekani kwa dola $699. Andy Rubin, ambaye ni miongoni mwa watu waliobuni programu ya software Android ya Goo… Read More
  • Vifaru vya Urusi vinavyotia wasiwasi mataifa ya Nato barani Ulaya Haki miliki ya pichaAFPImage captionArmata ni kifaru cha kisasa ambacho kinachukua nafasi ya vifaru vya enzi za muungano wa Usovieti Urusi imeunda vifaru vipya ambavyo vimeifanya Norway kuanza kufikiria upya mfumo wake wa k… Read More
  • Ndugai amkumbuka kwa majonzi Ndesamburo Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema anamkumbuka marehemu Phillemon  Ndesamburo aliyekuwa mbunge wa Moshi  Mjini (Chadema) kwa uchapakazi wake na mapenzi yake makubwa kwa wapiga kura wake.“Nimepokea kwa masikitiko t… Read More
  • Rais Magufuli amlilia Mwasisi wa Chadema Rais John Magufuli amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha  mmoja wa waasisi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema) Phillemon Ndesamburo huku akimtaja marehemu kuwa alikuwa kiongozi mwenye hekima na aliyez… Read More
  • Kambi ya Upinzani Bungeni uvunjwe MBUNGE wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbles Lema (Chadema), amelitaka Bunge kuvunja Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kutokana na maoni ya kambi hiyo kutosikilizwa.Lema amedai kuna kuchujwa kwa maneno yanayochangiwa na wabunge w… Read More

0 comments:

Post a Comment