Thursday, 8 June 2017

Nini kitafanyika sasa baada ya uchaguzi Uingereza?

Houses of ParliamentHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Nini kitafanyika kukikosekana mshindi wa moja kwa moja katika uchaguzi mkuu?
Chama chenye wabunge wengi kitaunda serikali?
Si lazima. Chama chenye wabunge wengi baada ya kura zote kuhesabiwa maeneo yote 650, huwa kinatangazwa mshindi na kiongozi wake huwa waziri mkuu. Lakini hili huenda lisifanyike wakati huu kwa kuwa chama kilichoshinda hakina wingi wa wabunge. Inawezekana kwa chama kilichomaliza cha pili kuunda serikali.
Mtu hushinda vipi uchaguzi?
Njia rahisi zaidi kwa mtu kuwa waziri mkuu ni chama chake kupata wingi wa wabunge katika Bunge la Commons - kuwa na wabunge wengi kuliko wabunge wote wa vyama hivyo vingine wakijumlishwa.
Unahitaji wabunge wangapi kuwa na wingi?
Idadi ya wabunge wanaohitajika ni 326. Wabunge hao watatosha kupitisha sheria mpya bila kushindwa an upinzani. Hilo likikosekana, huwa kuna bunge la mng'ang'anio.
Makadirio ya matokeo ya uchaguzi
Image captionMakadirio ya matokeo ya uchaguzi
Bunge la mng'ang'anio ni gani?
Ni wakati ambapo hakuna chaka hata kimoja kinachoweza kuwa na wingi wa wabunge kivyake. Hilo lilifanyika wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Kutatokea nini kukiwa na Bunge la mng'ang'anio tena?

Kutakuwa na msururu wa mashauriano kati ya viongozi wa vyama na wajumbe wao, wakijaribu kuunda serikali ya muungano au muungano wa kushindwa, kujaribu kusaidia kiongozi wa Conservative Theresa May au kiongozi wa Labour Jeremy Corbyn (watu wawili pekee kwa sasa walio na nafasi nzuri ya kuunda serikali) kuunda serikali.
Mmoja kati ya wawili hao anaweza pia kuamua kusimama kivyake na kujaribu kuunda serikali ya wachache, kwa kutegemea vyama vidogo anapohitaji kupitisha sheria mpya.

May, Corbyn. Sturgeon, FarronHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Nani atapata nafasi ya kwanza kuunda muungano?

Theresa May ataendelea kuwa waziri mkuu akiendelea kujaribu kuunda muungano wenyewe wabunge wengi.
Ikibainika kwamba hawezi, na Jeremy Corbyn anaweza, basi May atatakiwa kujiuzulu. Bw Corbyn naye atakuwa waziri mkuu wakati huo.
Lakini si lazima Corbyn asubiri hadi May amalize njia zake zote za kujaribu kuunda muungano kabla yake kuanza juhudi zake. Anaweza kushauriana na washirika watarajiwa wakati May naye akiendelea na mashauriano yake. Unaweza hata kupata wote wawili wanashauriana na vyama au viongozi sawa.
Hii itachukua muda gani?
Hakuna muda rasmi. Ilichukua siku tano mwaka 2010 kuunda muungano, lakini kawaida huchukua muda mrefu kuliko hivyo.
Mashauriano yanaweza kuendelea milele?
Kwa sasa, muda wa mwisho wa kwanza ni Jumanne tarehe 13 Bunge litakapokutana mara ya kwanza. Bi May ana hadi wakati huo kuunda muungano wa kumuwezesha kusalia madarakani au ajiuzulu, kwa mujibu wa mwongozo kutoka kwa afisi ya Baraza la Mawaziri.
Lakini Bi May lazima awe anafahamu kwamba Jeremy Corbyn anaweza kuunda serikali lakini yeye hawezi.

Na ikitokea iwe kwamba haibainiki iwapo serikali mpya inaweza kuundwa?

Njia pekee ya kufahamu iwapo serikali inaweza kuundwa ni iwapo ina imani na Bunge la Commons. Maana yake ni kwamba, je, serikali inaweza kupitisha sheria mpya zilizopendekezwa kwenye Hotuba ya Malkia? Hotuba ya Malkia inapangiwa kutolewa Jumatatu 19 Juni.
Theresa May anaweza kuamua kusalia na kubahatisha kuona iwapo anaweza kupata kura za kutosha kutoka kwa vyama vingine kupitisha sheria hizo.
Iwapo atakuwa amejiuzulu wakati huo na kumkabidhi Bw Corbyn nafasi, basi utakuwa mtihani kwa kiongozi huyo wa Labour kuonesha iwapo anaweza kuunda serikali.
Iwapo SNP watapata viti ambavyo wamebashiriwa kupata, wanaweza kutekeleza jukumu muhimu.
Msimamo wao umekuwa kwamba hawataunga mkono serikali ya Conservative.
Malkia hutekeleza wajibu gani?
Kiongozi wa chama anayeweza kumwambia Malkia kwamba ana idadi ya wabunge wa kutosha kuunda serikali ndiye atakayepewa idhini na Malkia kuunda serikali.
Malkia huwa hajihusishi na siasa, hivyo hakuna vile anavyoweza kumchagua waziri mkuu.
Kumekuwa na mapendekezo kwamba huenda Malkia akakosa kuwasilisha hotuba yake yeye binafsi iwapo kutakuwa na shaka kwamba huenda ikakosa kupitishwa.

Muungano ni nini?
David Cameron and Nick CleggHaki miliki ya pichaPA
Serikali ya Muungano huwa ni wakati vyama viwili ama zaidi vinashirikiana kuunda serikali moja. Washirika wenye wabunge wachache hugawiwa nyadhifa za mawaziri na pia mpango mmoja wa serikali hutayarishwa.

Serikali ya wachache huwa ni gani?
Commons chamber
Chama cha Conservatives au cha Labour kikashindwa kuunda muungano au kujisimamia kivyake kuunda serikali, kinaweza kuunda serikali ya wachache na kuteua mawaziri wake.
Chama hicho hakiwezi kupitisha sheria bila kura kutoka vyama vingine ambavyo havimo serikalini.
Mfano, Labour wanaweza kuunda serikali ya wachache ikiongoziwa na Jeremy Corbyn kama Waziri Mkuu, lakini chama hicho kitahitaji kura kutoka vyama vya Scottish National Party (SNP) na Liberal Democrat kupitisha sheria bungeni.

Chama kinachomaliza cha pili hivyo kinaweza kuunda serikali?

Ndio. Iwapo kuna shaka iwapo umma unaweza kuikubali serikali hiyo.

Kutakwua na uchaguzi mpya?

Ballot boxHaki miliki ya pichaPA
Awali, kunapoundwa serikali ya wachache, waziri mkuu baadaye huitisha uchaguzi mwingine nafasi nzuri inapojitokeza na kujaribu kupata wingi wa wabunge. Au, upinzani hushurutisha kufanyike uchaguzi mwingine kwa kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na serikali.
Ndipo uchaguzi mpya ufanyike hata hivyo itahitaji:
  • Theluthi mbili ya wabunge waunge mkono pendekezo la kuandaa uchaguzi. Hii in maana kwamba itabidi Labour na Conservative waunge mkono.
  • Kura ya kutokuwa na imani na serikali ipitishwe na wabunge wengi. Uchaguzi unaweza kufanyika katika chini ya siku 14 baada ya hapo serikali isipofanikiwa kushinda kura ya kutokuwa na imani nayo kabla ya muda huo kumalizika.

source:bbc

0 comments:

Post a Comment