Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mmoja wa Watu wanaoaminika kuwa ni Mbabe kama siyo Mtemi na Ngumi Jiwe wa kutukuka Kalapina jana wakati akihojiwa na Kipindi cha XXL kinachorushwa na Clouds fm aliamua kutema nyongo / kuvunja ukimya juu ya Kitendo cha Msanii mwenzake na mshikaji wake Roma Mkatoliki Kutekwa.
Kalapina ambaye anasifika mno kwa Usela / Uhuni na ukorofi ambao kiuhalisia kweli anauweza alianza kwanza kwa kumpa pole Roma Mkatoliki kwa yote yaliyomkuta ila hakusita pia kumlaumu kidogo Roma kwa kumwambia kuwa asingekubali kirahisi rahisi kubebwa na kuingizwa katika Gari na Kutekwa.
Ifuatayo ni nukuu Kuntu kabisa kutoka kwa Kalapina ambayo nadhani ni ujumbe tosha kwa Wazee wa Ununio mkabala na Mahaba Beach ( Watekaji )
“ Nakuambia Mimi nina hamu sana hao Watekaji siku wakosee tu waje waniteke Mimi kisha wajue kuwa kuna Watu tumebarikiwa kwa Ukorofi na Ukorofi tunaujua. Mimi wakija kama 10 na kutaka kuniteka basi nakuhakikishia lazima wakati wanafanikiwa kuniingiza katika Gari lao na kuniteka basi tayari name huku nyuma nitakuwa nimeshawaua Watatu au Wanne huku waliobaki nikiwaachia maumivu ya Kutukuka kabisa. Mdogo wangu Roma ulilegea sana na siku nyingine usifanye hivyo ukiona Mtu anataka kukuteka au ana nia mbaya nawe usimcheleweshe na badala yake mpe Kipondo / Kipigo pale pale “ mwisho wa kumnukuu Kalapina.
Friday, 16 June 2017
Home »
» Kalapina awapa salamu hizi waliomteka Roma Mkatoliki
Kalapina awapa salamu hizi waliomteka Roma Mkatoliki
Related Posts:
- Wasichana waliojifanya Waislamu wakamatwa NigeriaHaki miliki ya pichaAFPImage captionVazi la Hijab ni haki kwa wasichana wa Kiislamu kulivaa Wasichana saba waliojifanya kuwa Waislamu kwa kuvaa vazi la hijab wamekamatwa nchini Nigeria kwa kujaribu kufanya safari haramu ya ba… Read More
- Waziri wa Tamisemi atoa onyo hili kwa wakuu wa mikoa na wilaya Dodoma. Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amewaonya wakuu wa mikoa na wilaya kutotumia vibaya madaraka yao ya kukamata watu walio kwenye himaya zao.Ametoa onyo hilo leo (Ijumaa) … Read More
- Hizi ndizo adhabu za watuhumiwa wa Makinikia wakikutwa na hatia BAADHI ya wanasheria, wabunge waliomo katika kamati inayoshughulikia sheria na katiba na pia wachambuzi wa masuala ya kisheria, walisema kuwa yeyote miongoni mwa wanaochunguzwa sasa na vyombo vya dola anaweza kukumbana n… Read More
- Wahamiaji 1000 waokolewa pwani ya LibyaImage captionWahamamiaji huwa na imani ya kupata maisha bora zaidi Ulaya Vikosi vya uokoaji vinavyofanya kazi katika pwani ya Libya vimeokoa zaidi ya wahamiaji elfu moja kwa siku moja. Walikuwa katika boti dogo lililokuwa li… Read More
- Mpenzi wa jinsia moja achaguliwa waziri mkuu SerbiaHaki miliki ya pichaREUTERSImage captionAna Brnabic alichaguliwa na rais mpya , Aleksandar Vucic. Rais wa Serbia amemteua mwanamke ambaye ni mpenzi wa jinsia moja kuwa waziri mkuu katika jimbo la kihafidhana la Balkan. Ana B… Read More
0 comments:
Post a Comment