Sunday 28 May 2017

Askofu Gwajima: nitawavua mataulo wanaonichokoza

Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amewatahadharisha wanaomchokoza akisema ni sawa na mtu anayeanzisha ugomvi huku akiwa amevaa taulo.

Akihubiri leo, Gwajima amesema wakiendelea atawavua mataulo ili jamii iwaone.

Bila kufafanua kuhusu kauli hiyo, Gwajima amesema hawezi kunyamaza wakati watu wanaendelea kumfuata fuata.

"Leo nitakwapua mataulo ya   watu,"amesema huku akishangiliwa na waumini wake.

0 comments:

Post a Comment