Tanzania tumewahi kusikia mara kadhaa mabinti wakifukuzwa shule kwa kupata ujauzito wakiwa mashuleni lakini na mtu aliyempa ujauzito kufungwa, kumbe kwa Gabon ipo tofauti, ikitokea msichana akapata ujauzito akiwa shule anaendelea na masomo kama kawaida, Taarifa hii ni kwamujibu wa mtanzania anayeishi Gabon mzee Hamis Shaban Mwerani akizungumzia maisha ya Gabon.
“Kwa upande wa elimu kwa hapa Gabon msichana akiwa amepata ujauzito akiwa shuleni bado anaendelea na masomo kama kawaida hadi wakati wake wa kujifungua, kwa huku wala hutofika mahakamani ukimpa ujauzito mwanafunzi” >>> Hamis Shaban
source:muungwana
0 comments:
Post a Comment