Wednesday 31 May 2017

Reli mpya ya kisasa SGR yazinduliwa Kenya

Reli mpya ya SGR yazinduliwa Kenya
Image captionReli mpya ya SGR yazinduliwa Kenya
Kenya imezindua reli mpya kati ya mji wa Mombasa hadi Nairobi ikiwa ni miezi 18 mapema.
Reli hiyo iliotengezwa kupitia ufadhili wa shilingi bilioni 3.2 kutoka serikali ya China ndio mradi mkubwa wa miundo msingi kuwahi kutekelezwa na serikali tangu taifa hilo lijipatie uhuru wake.
Mradi huo umechukua takriban miaka mitatu na nusu kwa kutumia teknolojia ya ujenzi wa reli ya China kukamilika.
Wanawake watakaoendesha treni za kisasa Kenya
Reli hiyo inatarajiwa kuunganisha Sudan Kusini, DR Congo ,Burundi na Mombasa.
Reli mpya ya SGR iliozinduliwa na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Image captionReli mpya ya SGR iliozinduliwa na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Ni reli ya kwanza katika kipindi cha karne moja.
Safari ya kutoka Mombasa kuelekea Nairobi na treni ya kisasa itachukua saa nne na nusu ikilinganishwa na saa tisa kwa kutumia basi na saa 12 kwa kutumia treni ya zamani.
Nauli ya watu watakaokalia viti vya kawaida ni shilingi 900 huku wale watakaosafiri kwa kutumia business class wakilipa shilingi 3,000.
Rais Uhuru Kenyatta alisema wakati wa uzinduzi wa reli hiyo ambayo imeanzishwa mwamko mpya katika historia ya Kenya.
Behewa la Ist Class ambalo Wakenya watakaosafiria watalipa shilingi 3000
Image captionBehewa la Ist Class ambalo Wakenya watakaosafiria watalipa shilingi 3000
''Historia ilianzwa miaka122 iliopita wakati Waingereza waliokuwa wametawala taifa hili walipoanzisha treni hiyo iliokuwa haijulikani inakokwenda na kupewa jina Lunatic Express
''Leo licha ya kukosolewa pakubwa tunasherehekea Madaraka Express {ikitajwa baada ya siku ambayo Wakenya walijipatia uhuru wao kikamilifu} badala ya Lunatic Express.
Gharama ya mradi huo imekosolewa na upinzani ambao unasema mradi huo umeigharimu Kenya fedha nyingi mno.
Vilevile wamemshutumu rais Kenyatta kwa kuomba fedha kutoka China bila mpango.
Serikali nayo inasema kuwa ni sharti iwekeze katika miundo msingi ili kuvutia wawekezaji.

source:bbc

0 comments:

Post a Comment