Wednesday, 24 May 2017

Trump asababisha Al Jazeera kufungiwa Saudi Arabia

Saudi Arabia imeifungia mitandao ya Al Jazeera na Magazeti ya Qatar baada ya Rais wa Qatar Tamim Bin Hamad Al-Thani kusema anaishangaa Saudi Arabia kumkaribisha Rais wa Marekani Donald Trump kauli iliyopingwa na Mfalme wa Saudi Arabia.

Sehemu ya taarifa ya Rais wa Qatar kupinga ziara ya Trump Saudi Arabia ilisomeka: >>>“Rais Trump hawezi kukaribishwa Qatar na ninaishangaa Saudi Arabia kumkaribisha mtu kama Trump ambaye anashtakiwa kwa makosa ya kihalifu nchini kwake. Mimi naitambua Serikali ya Iran kama Serikali ya Kiislamu kama Marekani haiitambu si lazima kukubaliana nao.”

Mtandao wa Al Jazeera umefungiwa kwa sababu unamilikiwa na Serikali ya Qatar jambo ambalo limewafanya watumiaji wa mtandao huo Saudi Arabia kupata shida ambapo kila wakijaribu kuingia kwenye mitandao hiyo wamekuwa wakikutana na ujumbe uliowatahadharisha kuwa mitandao hiyo imefungiwa.

0 comments:

Post a Comment