Msanii wa Nikki wa Pili, amempongeza Rais Magufuli kwa kitendo alichokifanya leo cha kumtumbua Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo na kumwambia Mungu amsimamie katika kupambana na ufisadi.
Niki ametoa salamu hizo za pongezi kupitia ukurasa wake wa kijamii instagram kwa kusema watanzania wanaopewa dhamana wasipoamua kuwa waadilifu umaskini utaweza kuandika historia tukufu kwa Tanzania.
"Wizi mkubwa utamkuta mwekezaji na wakala wake wa kitanzania (wasomi, viongozi, wafanya biashara) yaani ni kama ule uchumi wa kikoloni manufaa ni kwa kampuni ya nje na kitabaka cha watanzania wachache...Nimpongeze Mkuu wa nchi kwa kuamua kupambana na ufisadi huu...Ila vita ya kuvunja mfumo wa kiuchumi wa kifisadi ni hatari...Kina Lumumba, Sankara huko Chile, Nikaragwa, Venezuela, Haiti, Iran...Viongozi hawakupona ni vita kuu Mungu akusimamie". Ameandika Nikki wa Pili.
0 comments:
Post a Comment