Sunday 28 May 2017

Taarifa ya leo Mei 28, kumuhusu Ivan aliyekuwa Mume wa Zari

IVAN SEMWANGA, aliyekuwa mume wa Zarina Hassan ‘The Bosslady’ ambaye sasa ni mpenzi na mzazi mwenzake wa mwanamuziki wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnum’, atazikwa Jumanne (Mei 30) wiki ijayo  nyumbani kwao Kayunga, Uganda.

Mwili wa mwananchi huyo wa Uganda aliyefariki nchini Afrika Kusini kutokana na matatizo ya moyo, umewasili leo nchini Uganda ambako leo utafanyiwa mkesha maalum na Jumatatu kufanyiwa ibada maalum ya wafu katika Kanisa la Namirembe siku ya Jumatatu.

Semwanga alijipatia umaarufu mkubwa tangu nchini mwake Uganda hadi Afrika Kusini ambako ameacha utajiri mkubwa uliomfanya kuwa mmoja ya watu matajiri nchini humo kabla ya kufikwa na mauti.

0 comments:

Post a Comment