Sunday 28 May 2017

Bomba la kupitisha pombe kujengwa Ujerumani

Pombe itakuwepo kwa wingi katika tamasha hiloHaki miliki ya pichaAFP
Image captionPombe itakuwepo kwa wingi katika tamasha hilo
Waandalizi wa Tamasha maarufu la muziki wa rock nchini Ujerumani wamewahakikishia wateja zaidi ya elfu 75 kwamba, katu! hawatokumbwa na kiu ya pombe.
Wanajenga bomba kubwa la kusafirisha pombe katika eneo la tamasha hilo.
Waandalizi wa tamsha hilo maarufu kwa jina, Wacken Open Air festival, wanasema bomba hilo litakuwa na uwezo wa kufikisha glasi sita za pombe kwa kila sekunde.
Bomba hilo litakuwa na urefu wa kilomita 7 na upana wa inchi 14.
Bomba hili litazuia uharibifu unaotokana na mgari ya kusafirisha pombe kila sikuHaki miliki ya pichaWOA WEBSITE
Image captionBomba hili litazuia uharibifu unaotokana na mgari ya kusafirisha pombe kila siku
Watu elfu 75 huwa wanahudhuria tamasha hilo kila mwaka, na inakadiriwa kwamba kila mmoja huwa anabugia lita tano za pombe katika kipindi cha siku tatu.
Zaidi ya watu 75,000 huwa wanahudhuria tamasha hilo kila mwakaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionZaidi ya watu 75,000 huwa wanahudhuria tamasha hilo kila mwaka

0 comments:

Post a Comment