Monday, 29 May 2017

Korea Kaskazini yarusha kombora jingine kuelekea Japan

Jaribio hilo limetekelezwa siku moja baada ya taarifa kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alisimamia jaribio la teknolojia ya kudungua ndege 28 Mei 2017.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJaribio hilo limetekelezwa siku moja baada ya taarifa kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alisimamia jaribio la teknolojia ya kudungua ndege za kivita
Korea Kaksazini imerusha kombora la masafa mafupi, ambalo ni la tatu kurushwa na taifa hilo katika kipindi cha wiki tatu.
Kombora hilo aina ya Scud lilipaa umbali wa kilomita 450 (maili 280) kabla ya kuanguka katika maeneo ya bahari ya Japan, hatua iliyoifanya Japan kulalamika vikali.
Wachanganuzi wanasema jaribio hilo ni ishara kwamba Korea Kaskazini inapiga hatua katika kuunda makombora yanayoweza kubeba mabomu.
Korea Kaskazini imeendelea kukiuka azimio la Umoja wa Mataifa linaloizuia kufanya majaribio yoyote ya makombora au silaha za nyuklia, na imeongeza kasi na idadi ya majaribio hayo katika miezi ya karibuni.
Kikosi cha Jeshi la Marekani Bahari ya Pasifiki kimesema kombora hilo lilirushwa kutoka Wonsan, Korea Kaskazini na lilipaa kwa karibu dakika sita kabla ya kuanguka.
Waziri kiranja wa Japan Yoshihide Suga amewaambia wanahabari kwamba kombora hilo lilianguka katika eneo la bahari lililo kati ya visiwa vya Sado na Oki nchini Japan, katika eneo la pamoja la kiuchumi la visiwa hivyo viwili.
Map showing Oki and Sado in Japan, and Wonsan in North Korea
Msemaji wa jeshi la Korea Kusini amesema kombora hilo lilipaa juu hadi kilomita 120 angani, na utathmini unaendelea kubaidi "idadi hasa ya makombora yaliyorushwa," ishara kwamba huenda nchi hiyo ilirusha zaidi ya kombora moja.
Jariibo hilo la kombora limetekelezwa siku moja baada ya vyombo vya habari vya serikali nchini Korea Kaskazini kusema nchi hiyo lilifanyia majaribio mfumo mpya wa kudungua ndege za kivita, na kutoa picha za kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un alishuhudia majaribio hayo.
Kim Jong-un.Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionKim Jong-un (akiwa na shati la rangi jeupe) anadaiwa kushuhudia kufanyiwa majaribio kwa mfumo mpya wa kudungua ndege za kivita
Korea Kaskazini ina hazina kubwa ya makombora ya masafa mafupi aina ya Scud ambayo yaliundwa na Muungano wa Usovieti.
Makombora ya kisasa ya Scud yanaweza kufika umbali wa kilomita 1,000.
Majaribio mawili ya majuzi yaliyofanywa na Korea Kaskazini, ambayo ilisema yote yalifanikiwa, yalikuwa ya makombora ya masafa ya wastani na masafa marefu.
Korea Kaskazini ilisema jaribio la kwanza lilikuwa la kombora jipya lenye uwezo wa kubeba kichwa cha bomu la nyuklia.
Mifano ya makombora ya Scud yanayomilikiwa na Korea Kaskazini Septemba 5, 2016.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMifano ya makombora ya Scud yanayomilikiwa na Korea Kaskazini
Pyongyang imekuwa ikifanyia majaribio makombora kwa kasi sana, na wataalamu wanasema huenda inakaribia kufanikiwa kumiliki kombora la masafa marefu linaloweza kufikia maeneo ya Marekani bara.
Korea Kaskazini imekuwa ikisema mpango wake wa kustawisha silaha unanuiwa kukabili hatari kutoka kwa uchokozi wa Marekani.
Uwezo wa makombora ya Korea Kaskazini
Makombora ya Korea Kaskazini


source:bbc

0 comments:

Post a Comment