Home »
» Mpoto aachiwa kitu na marehemu mzee Ngosha wa nembo ya taifa
Msanii wa muziki wa kughani nchini Tanzania, Mrisho Mpoto amesikitishwa na kifo cha Mzee Francis Kanyasu aliyechora Nembo ya Taifa na kusema anatamani siku zirudi nyuma ili aweze kuongea naye tena.
Mpoto amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa instagram kwa kudai Mzee huyo alishawahi kumsaidia kumpa wazo la kufanya video ya wimbo wake wa 'Njoo ichukue'.
"Hii ni taarifa ya kunisikitisha sana kwenye maisha yangu ya muziki, nakumbuka kabla ya kutoa wimbo wa 'Sizonje' nyuma yake nilitoa 'Njoo nichukue' huyu Mzee alikuja ofisini kwangu kuniambia maneno mazito sana kwamba anapenda kazi yangu na alinitabiria mambo mengi mazuri kwenye safari yangu ya maisha nanukuu YACHUKULIE MANENO HAYA NI YA CHIZI KAONGEA" aliandika Mpoto.
Aidha Mpoto aliendelea kusema kuwa "Ombi lake lilikuwa moja tu alitamani kufanya kazi na mimi, ofisi nzima ikamchukulia kama mzee aliyechanganyikiwa wakataka kumfukuza, mlinzi wetu wa ofisi akasema msimpuuze mpeni nafasi, tulipompa nafasi ndiyo akatoa wazo la video ya wimbo wa 'Njoo uichukue' iweje, na akasema yule mzee Mshuba kikongwe muuza bangi ataigiza yeye mwenyewe tulicheka Sana maana wazo lake lilikua zuri na liliungwa mkono na 'Director' Adamu Juma"
Pamoja na hayo Mpoto amesema baada ya kupata taarifa ya kifo ndipo alipokuja kugundua kuwa Mzee Francis anamfahamu vizuri.
"Baada ya kuangalia kwa makini kumbe ndiyo yule mzee aliyefariki leo mchora Nembo ya Taifa, natamani siku zirudi nyuma niongee naye tena, roho imeniuma sana kwa kweli sijui hata nifanye, nini kibaya zaidi baada ya 'shooting' alitutoroka hata hatukujua tutampataje".alisisitiza Mpoto
SOURCE:MUUNGWANA
Related Posts:
Dwayne 'The Rock' Johnson kuwania urais Marekani mwaka 2020?Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMwigizaji na mwanamiereka Dwayne 'The Rock' Johnson
Dwayne 'The Rock' Johnson kuwania urais mwaka 2020?
Dwayne 'The Rock' Johnson alitangaza kuwa atawania urais wa Marekani mwaka … Read More
Bomba la kupitisha pombe kujengwa UjerumaniHaki miliki ya pichaAFPImage captionPombe itakuwepo kwa wingi katika tamasha hilo
Waandalizi wa Tamasha maarufu la muziki wa rock nchini Ujerumani wamewahakikishia wateja zaidi ya elfu 75 kwamba, katu! hawatokumbwa na kiu ya … Read More
Gavana asema al-Shabab huenda wakateka eneo la KenyaImage captionRamani ya Somalia
Viongozi wa eneo la mashariki nchini Kenya wameonya kwamba maeneo ya taifa hilo huenda yakanyakuliwa na wapiganaji wa Al-Shabab.
Gavana wa kaunti ya Wajir ambayo inapakana na taifa la Somalia a… Read More
Marekani kufanya majaribio ya kudungua komboraImage captionMfumo wa kudungua makombora wa Marekani uliopelekwa Korea Kusini
Idara ya jeshi nchini Marekani kwa mara ya kwanza itajaribu kudungua kombora la masafa marefu lililo na uwezo wa kufyatuliwa kutoka bara moja hadi … Read More
Trump 'atengwa' na wenzake G7Image captionRais Trump ametengwa na wenzake kuhusiana na makubaliano ya tabia nchi yaliofakiwa mjini Paris
Viongozi katika mkutano wa G7 wametofautiana kuhusu taarifa ya mabadiliko ya tabia nchi.
Viongozi sita walikubaliana… Read More
0 comments:
Post a Comment