Tuesday, 23 May 2017

Wanafunzi 3 kutoka Tanzania wafariki Ziwa Victoria

Wanafunzi hao walikuwa wanerejea nyumbani
Wanafunzi watatu kutoka shule ya msingi ya Butwa mkoani Geita wamekufa maji huku wenzao tisa wakinusurika kifo baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kupinduka katika Ziwa Victoria.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo amesema tukio hilo lilitokea Jumatatu jioni wakati wanafunzi hao wakitoka shuleni kuelekea nyumbani kitongoji cha Lulegeya
Amesema wanafunzi hao ambao wote ni wasichana wana umri kati ya miaka 9 hadi 13. Miili yote imepatikana na kukabidhiwa kwa familia zao.
Akielezea tukio lilivyotokea, Kamanda Mwabulambo anasema wakiwa katikati ya maji, nahodha wa mtumbwi huo uliokuwa umebeba wanafunzi 12 alihofia idadi ya abiria kuwa ni kubwa na hivyo kuamua kurudi nchi kavu ili apunguze abiria hao.
Lakini kabla ya kufika nchi kavu, baadhi ya wanafunzi walihamia upande mmoja wa mtumbwi na kusababisha uzito kuzidi na ndipo mtumbwi huo ulipopinduka umbali wa mita 20 kutoka nchi kavu.
Wanafunzi tisa wa kiume walifanikiwa kuogelea hadi kufika nchi kavu na kuokoa maisha yao.
Kamanda Mwabulambo amesema polisi inamshikilia mmiliki wa mtumbwi huo uliopinduka kwa mahojiano zaidi kujua undani wa ajali hiyo.
Mtumbwi ndio njia kuu ya usafiri katika visiwa vilivyopo Ziwa Victoria lakini mingi ipo katika hali mbaya na hivyo kusababisha ajali za mara kwa mara.

source:bbc

Related Posts:

  • Nape amemjibu Makonda, Picha limeanza upyaaa Siku moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuhojiwa na kituo cha Star Tv kuhusu mambo kadha wa kadha likiwemo suala la uvamizi wa Clouds Media na kusema Hakupaswa kumuingilia kwakuwa wote ni watumishi... Basi Nape ame… Read More
  • Polisi watangaza dau la Mil. 60 Ukiwakamatisha hawa JESHI la Polisi mkoa wa Pwani limetangaza zawadi ya Sh. milioni tano kwa mwananchi ambaye atafanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa 12 ambao limedai wanajihusisha na mtandao wa mauaji yanayoendelea katika Wilaya za Kibiti, Mku… Read More
  • Mbunge atinga bungeni na rundo la risiti Dodoma.Mbunge wa Viti maalum (Chadema), Rhoda Kunchela aliwasilisha bungeni furushi la risiti za mwenge wanazodaiwa kuchangishwa kwa nguvu, walimu na wafanyabiashara.Mbunge Kunchela aliomba kutoa hoja ili ijadiliwa na Bunge … Read More
  • Madhara ya Mvua ya siku sita yaua 10, yabomoa nyumba 44 Tanga. Tathmini ya madhara yaliyotokana na na mvua zilizonyesha kwa siku sita mfululizo wiki iliyopita mkoani hapa zimeonyesha kuwa hadi sasa watu 10 wamekufa huku  nyumba 44 zikibomoka na nyingine 218 zikizingirw… Read More
  • Nyumba zateketea kwa moto Sengerema Sengerema. Nyumba za wavuvi ambazo idadi yake haijajulikana hadi sasa katika kisiwa cha uvuvi cha Nyamango Kata ya Bulyaheke  halmashauri ya Buchosa wilayani hapa, zinateketea kwa moto ambapo chanzo chake hakijajul… Read More

0 comments:

Post a Comment