Tuesday 23 May 2017

Muungano wa wafanyakazi wampiga marufuku rais Zuma

Muungano wa wafanyikazi nchini Afrika Kusini Cosatu
Image captionMuungano wa wafanyikazi nchini Afrika Kusini Cosatu
Baraza la Muungano wa wafanyikazi nchini Afrika Kusini Cosatu ambalo ni mshirika mkuu wa chama tawala cha ANC limempiga marufuku rais Jacob Zuma kuhutubia katika mikutano yake.
Akisoma taarifa kwa vyombo vya habari siku ya Jumanne baada ya mkutano mkuu wa baraza hilo, katibu mkuu wa Cosatu Bheki Ntshalintshali alisema: Rafiki Jacob Zuma hataruhusiwa tena kuhutubia katika Cosatu.
Bwana Zuma alizomewa katika mkutano wa wafanyikazi wa mwezi Mei ulioandaliwa na Cosatu mapema mwezi huu.
Chama cha ANC kimegawanyika kabla ya kufanyika kwa mkutano wake wa kila mwaka ambapo rais Zuma anatarajiwa kujiuzulu kama kiongozi wa chama.
Rais Jacob Zuma apigwa marufuku na COSATUHaki miliki ya pichaAFP
Image captionRais Jacob Zuma apigwa marufuku na COSATU
Muungano huo ambao ni mkubwa umesisitiza wito wake kwamba haumuungi mkono tena rais Zuma.

0 comments:

Post a Comment