Dar es Salaam. Uamuzi wa Serikali kuhusu suala la usafirishaji wa mchanga wa madini, utategemea ripoti ya kamati ya pili iliyoundwa na Rais John Magufuli kuchunguza suala hilo.
Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Gerson Msigwa ikiwa ni siku moja baada ya kampuni ya Acacia kuitaka Serikali kuunda kamati huru kuchunguza kiasi cha madini kwenye makontena yake 277 yaliyozuiwa bandarini.
Wiki iliyopita, Rais Magufuli alikabidhiwa ripoti na kamati ya kwanza iliyoongozwa na Profesa Abdulkarim Mruma ambayo ilibaini kuwa makontena hayo yana tani 7.8 za dhahabu.
Pia, Acacia wanadai hawakupewa ripoti ya kamati hiyo licha ya kutoa ushirikiano wakati wa uchunguzi.
“Sijui chochote kuhusu hao Acacia kuomba iundwe kamati huru, lakini tunasubiri ripoti ya kamati ya pili iliyoundwa kuchunguza sakata hili wampelekee ripoti Rais,” alisema Msigwa.
Wakati Ikulu ikisema hayo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alizungumzia ripoti ya kamati ya Profesa Mruma na kusema chanzo cha hayo ni sheria mbovu za madini pamoja na mikataba iliyotungwa katika kipindi cha utawala wa Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa. “Tanzania inaruhusu kupitishwa kwa sheria mbovu na wizi halafu baadaye wanapiga kelele, wapinzani tunasema sheria zote lazima zifumuliwe na kupangwa upya,” alisema.
Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai alionyesha shaka kuwa ni lazima Taifa litaingia kwenye migogoro mikubwa ya kidiplomasia kutokana na ukiukwaji wa sheria unaofanywa ikiwamo sakata la mchanga huo.
Alisema itachukua muda mrefu kwa wawekezaji kuiamini tena Tanzania na kuja kuwekeza kwa kuwa hata waliopo wameanza kuondoka.
Pia, Mbowe alisema kuna tetesi kuwa uchunguzi huo ambao ulimng’oa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo una upungufu mwingi.
Suala la fedha nalo limeibuka katika sakata hilo.
Akizungumzia suala hilo, aliyekuwa mjumbe wa Mpango wa Uhamasishaji wa Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi na Mafuta (Teiti), Bubelwa Kaiza alisema ipo haja ya kupitiwa upya kwa taarifa za fedha za kampuni za madini ambazo zilikuwa zikiwasilishwa.
Kaiza alisema kwa mujibu wa ripoti ya kamati ya kuchunguza mchanga wa madini iliyowasilishwa siku chache zilizopita ni wazi kampuni hizo hazikuwa zikitoa taarifa sahihi.
Alisema Teiti ilikuwa inapitia taarifa za fedha ambazo zilikuwa zinawasilishwa kwa hiari na kampuni husika na si kuchunguzwa, hivyo upo uwezekano walikuwa wanatumia mwanya huo kutoa taarifa za uongo.
source:muungwana
Sunday, 28 May 2017
Home »
» Ikulu yatoa majibu haya kwa Acacia
Ikulu yatoa majibu haya kwa Acacia
Related Posts:
Korea Kaskazini yalifanyia majaribio kombora lingine Ndege mbili za kijeshi za China zimeizuia 'vibaya' ndege ya Marekani kulingana na jeshi la Marekani. Ndege hiyo inayohusika na kufanya uchunguzi, ilikuwa katika safari yake ya kutaka kugundua mionzi katika anga ya kimataif… Read More
Majasusi wa Marekani wauwawa na China Gazeti la New York Times limeripoti kuwa China, imewauwa au kuwafunga jela majasusi kati ya 18 au 20 hivi wa CIA, katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na kulemaza kabisa shughuli za Marekani za kuichunguza China. Afis… Read More
How to Start a Cooking Distribution Business in Tanzania: Details Requirement Cooking gas becomes so popular fuel for cooking. Have you ever wondered why is everyone using gas for cooking now?. The answers are pretty simple. The first thing first, cooking gas is environment-frie… Read More
Marufuku ya uuzaji wa nyama ya mbwa yasababisha wasiwasi China Sherehe ya kula nyama ya mbwa nchini China ilio na umaarufu kwa ukatili wa wanyama mwaka huu itapigwa marufuku kuuza nyama ya mbwa. Ulaji wa mbwa nchini China sio haramu na wauzaji wa nyama hiyo tayari wameanza kulalamikia… Read More
SIMU YAMPONZA:Mwanamume amshtaki mwanamke aliyetumia simu akichumbiwa MarekaniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES Mwanamume mmoja katika jimbo la Texas, Marekani anadaiwa kuwashtaki mwanawake ambao aliyekuwa amemlipia wakatazame sinema walipokuwa wanachumbiana lakini akaanza kutumia simu yake kutuma ujumb… Read More
0 comments:
Post a Comment