Wednesday 31 May 2017

Imevujaa!! Kumbe John Bocco alikuwa anahitajika Azam

Golikipa namba moja wa Azam FC Aishi Manula amesema, John Bocco ‘Adebayor’ bado alikuwa anahitajika ndani ya kikosi cha Azam.

Manula amesema, licha ya timu yake kusajili wachezaji wengi wa kigeni miaka ya hivi karibuni bado Bocco amekuwa mhimili muhimu ndani ya timu yao kutoka na uwezo wake wa kutupia kambani.

“Unapokuwa na mtu kama Bocco katika timu ni kitu kikubwa sana kwa sababu ametoka mbali na Azam na amefanya mengi makubwa, makombe mengi yaliyopatikana ndani ya Azam FC  nadhani ni katika uongozi wake yeye kama nahodha, ni mtu muhimu sana.

“Bocco ni mchezaji ambaye bado alikuwa anahitajika katika klabu ya Azam, kwa sababu unaweza ukaona wachezaji wengi wanaokuja Azam katika nafasi yake hawafanyi vizuri. Wamesajiliwa wachezaji wengi professional waje waisaidie klabu na hawaisaidii mara zote Bocco anakuwa mkombozi na tegemeo.”

“Kitu cha kufikiria ni kwamba, leo Bocco anaondoka nani anakuja? Tunamuona Shabani Idd anakuja vizuri lakini bado ni kijana mdogo anahitaji support kubwa kutoka Bocco kama alivyokuwa anapewa awali. Nilikuwa nawaona wanakaa pamoja na kuzungumza, tukiwa mazoezini anajaribu kumuelewesha kwahiyo walikuwa ni marafiki.”

“Kuondoka kwa Bocco yule kijana anabaki pekeake kusimama mwenyewe itamuwia vigumu. Bocco anaondoka akiwa anategemewa kama top striker na utaona hata wakati yupo nje anasumbuliwa na majeraha timu ilikuwa inayumba.”

“Bocco kaondoka Azam kwa sababu ya maslahi yake hajaondoka kwa sababu Azam wamemchoka au hawahitaji tena kuwa na yeye kwa sababu uwezo wake umeshuka, uwezo wake haujashuka licha ya kusumbuliwa na mejeruhi.”

“Namtakia maisha mema huko anapokwenda na hata tukikutana nadhani hakutakuwa na uadui kwa sababu soka si uadui.”

Juma lililopita afisa habari wa Azam FC Jafar Idd alithibitisha klabu hiyo kuachana rasmi na Bocco baada ya mshambuliaji huyo kudumu kwa muda mrefu ndani ya Azam.

0 comments:

Post a Comment