Thursday 25 May 2017

Prof. Maghembe ataka walionyang’anywa pikipiki warudishiwe


Responsive image
Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe akijibu hoja mbalimbali za Wabunge waliochangia bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018.

Serikali imeagiza kurejeshwa mara moja kwa pikipiki, baiskeli na vifaa vyote vya wananchi vilivyokamatwa katika maeneo mbalimbali nchini baada ya wamiliki wake kubainika kujihusisha na uchomaji na uuzaji wa mkaa.
Kauli hiyo ya Serikali imetolewa Bungenni Mjini Dodoma na Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe wakati akijibu hoja mbalimbali za Wabunge waliochangia bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018.
Kuhusu Watanzania ambao wamekua wakijihusisha na kilimo cha mashamba ya miti ama misitu, Waziri Maghembe amesema kuwa  Wakulima hao wako huru kujichagulia matumizi ya miti yao.
Bunge limepitisha bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa Fedha wa 2017/2018 baada ya kujadiliwa na Wabunge kwa takribani siku Mbili na hoja zao mbalimbali kujibiwa na serikali.


0 comments:

Post a Comment