Sunday, 28 May 2017

Wauawa kwa kuwalinda wanawake Waislamu Marekani

Polisi wanasema mwanamume aliyekuwa akitukana, aliwageukia wanaume hao waliojaribu kuingilia katiHaki miliki ya pichaCBS/EVN
Image captionPolisi wanasema mwanamume aliyekuwa akitukana, aliwageukia wanaume hao waliojaribu kuingilia kati
Polisi katika mji wa Portland nchini Marekani, wanasema wanaume wawili waliuawa, walipojaribu kumzuia mwanamume aliyewatukana kiubaguzi, wanawake wawili, walioonekana kuwa Waislamu.
Kisa hicho kilitokea kwenye treni jana.
Polisi wanasema mwanamume aliyekuwa akitukana, aliwageukia wanaume hao waliojaribu kuingilia kati, na kuwadunga visu na kuwauwa.
Abiria mwengine alijeruhiwa, kabla ya mshambuliaji kukamatwa.
Halmashauri ya uhusiano baina ya Marekani na Waislamu, imesema Rais Trump lazima atoe kauli kulaani chuki inayozidi dhidi ya Waislamu.
Imesema hali inazidi kuwa mbaya kwa sababu ya maneno ya rais na sera zake.

Related Posts:

  • Nyalandu: Majeruhi wa Lucky Vicent kuruhusiwa Hospotali kesho Hospitali ya Mercy ya Marekani,  imebainisha kuwa  huenda watoto wawili majeruhi wa ajali ya gari la Shule ya Lucky Vincent wakaruhusiwa kutoka hospitali wakati wowote kuanzia kesho.Mbunge wa Singida Kaskazini, La… Read More
  • Ujumbe wa Diamond Baada ya Ivan kufariki Dunia Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond Platnumz ameandika ujumbe huu "Mbele yako, Nyuma yetu" Ujumbe huo ni baada ya Aliyekuwa mume wa Zarina Hassan ‘Zari The Bosslady’, Ivan Semwanga kufariki dunia akiwa hospitali nchi… Read More
  • Meri ya kivita ya Marekani imeonakana karibu na visiwa vya Uchina Maafisa wa Marekani wanasema manowari ya wanamaji wa Marekani imetekeleza oparesheni maalum ya 'uhuru wa ubaharia' karibu na visiwa vinavyozozaniwa vya bahari ya kusini mwa china. Oparesheni hiyo karibu na kisiwa kimoja… Read More
  • Professa Muhongo amemuibua Kafulila Alikuwa Mbunge Kigoma Kusuni,  David Kafulila ameibuka na kutoa kauli yake maamuzi yaliyofanywa na Rais Magufuli baada ya kupokea ripoti ya Kamati Maalum kuhusiana na uchunguzi wa makontena 272 ya makinikia yaliyokuwa … Read More
  • "Manji anatikisa kibiriti" Katibu wa baraza la wazee wa Yanga Mzee Ibrahim Akilimali amesema, huenda kujiuzulu kwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji ni kutikisa kibiriti tu lakini atarejea tena kwenye nafasi yake kwa sababu tayari alishawahi kuta… Read More

0 comments:

Post a Comment