Tuesday, 30 May 2017

Mbunge Peter Serukamba asema Rais Magufuli ataigwa duniani kote

Mbunge wa Kigoma Vijijini (CCM), Peter Serukamba amefunguka na kusema jambo alilofanya Rais Magufuli kuzuia mchanga litakwenda kuigwa duniani kote na kuleta mapinduzi katika 'Extractive Industries' kwa kazi kubwa aliyofanya.

Serukamba alisema hayo jana bungeni na kusema ukiona mpinzani wako anakupinga katika jambo lolote lile basi ujue umefanya jambo ambalo ni sahihi ila ukiona mpinzani wako anakusifu ujue umefanya jambo baya, hivyo kwa kuwa wapinzani wanalalamika basi Rais amepatia katika maamuzi yake, na anatakiwa kupewa ushirikiano wa wananchi na wabunge.

"Mimi kama mwanasiasa ukiona mtu ambaye ni adui yako umefanya jambo akakusifia ujue lipo tatizo, ila ukiona umefanya jambo adui yako akasema umekosea maana yake umepatia sana. Mimi naomba nimpongeze Rais Magufuli kwa kazi kubwa aliyofanya na niwaambie waheshimiwa wabunge, duniani kote 'Extractive Industries' inaenda kubadilika atakaye kuwa kwenye historia ya kubadilisha Extractive Industries ni Rais Magufuli, leo duniani kote kila kwenye migodi mambo yatabadilika kwa sababu ya Magufuli amefungua milango, niwaambieni watanzania tusiogope kwenye hili lazima tuwe nyuma ya Rais tumuunge mkono aendelee na nina hakika wawekezaji watakuja mezani" alisisitiza Serukamba 

Related Posts:

  • MWIGULU ATETA NA POLISI MAUAJI KIBITI WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amefanya ziara ya kushtukiza wilayani Kibiti mkoani Pwani na kuteta kwa faragha na askari wa operesheni maalumu ya kuwasaka wauaji. Alisema  mauaji sasa yametosha … Read More
  • Tamko la mradi wa bomba la mafuta ghafi lasainiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni wakitia saini tamko la pamoja la kukamilika kwa majadiliano na vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima… Read More
  • Libya yakabiliwa na vita vya ndani Taarifa kutoka nchini Libya zinaelez kwamba jeshi liloljitangaza kuwa la taifa hilo, ambalo linaunga mkono mamlaka yenye makao yake katika mji wa mashariki wa Tobruk,limefanya mashambuliuzi kadhaa ya anga dhidi ya vikosi pi… Read More
  • Mwanamke akata uume wa kiongozi wa dini India   Mwanamke mmoja wa umri wa miaka 23 nchini India amekata uume ya wa kiongozi mmoja wa dini kwenye jimbo lililo kusini mwa nchi la Kerala, akidai kuwa alimbaka kwa miaka kadha. Polisi wanasema kuwa kiongozi huyo wa d… Read More
  • FEDHA ZA RAMBIRAMBI ZATUMIKA KUJENGA HOSPITALI JINAMIZI la matumizi ya fedha za rambirambi kwenda kwa familia za wanafunzi limegeuka kaa la moto kwa kuamuliwa sehemu ya fedha hizo zipelekwe kukarabati Hospitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru. Fedha hizo ni zinazotakiw… Read More

0 comments:

Post a Comment