Sunday 28 May 2017

Dwayne 'The Rock' Johnson kuwania urais Marekani mwaka 2020?

Mwigizaji na mwanamiereka Dwayne 'The Rock' JohnsonHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMwigizaji na mwanamiereka Dwayne 'The Rock' Johnson

Dwayne 'The Rock' Johnson kuwania urais mwaka 2020?

Dwayne 'The Rock' Johnson alitangaza kuwa atawania urais wa Marekani mwaka 2020 wakati akitumbuiza mashabiki wake katika kipindi maarufu cha Saturday Night Live.
Mwigizaji maarufu Tom Hanks alikubali kuwa naibu rais.
Baadaye, mwigizaji huyo anayelipwa mshahara mkubwa zaidi ulimwenguni alisema tangazo hilo lilikuwa la utani.
Hata hivyo alisisitiza kwamba "Marekani inahitaji viongozi walio na uwezo wa kuongoza, wanaojali maslahi ya taifa hili na raia wake"

0 comments:

Post a Comment