Tuesday 30 May 2017

Basi la Falcon lapata ajali Uganda, Watanzania 27 wajeruhiwa

Dar es Salaam. Watanzania 27 wamejeruhiwa katika ajali ya basi kampuni ya Falcon walilokuwa wakisafiria kutokea Tanzania kuelekea Uganda, baada ya kuangukia upande wa kushoto njia kuu ya Masaka, Uganda.

Abiria hao walikuwa njiani kuelekea Namugongo katika sherehe za siku ya Martyrs ambayo ahudhimisha na waumini wa Kanisa Katoliki kote duniani kila ifikapo Juni 3.

Polisi nchini Uganda wanasema basi hilo lenye usajili namba T967-BTA lilishindwa kupanda mlima iliyopo kati ya eneo la Kyatera na Masaka baada ya breki ya gari hizo kufeli na kusababisha ajali.

Hata hivyo polisi hao wamesema hakuna majeruhi walio kwenye hali mbaya.

Miongoni mwa waliojeruhiwa ni Maria Ngonyari, Robert Imman (40),  Alex Rono (64), Angela Kigulwe Biringi (65), Gloria Mwisa (29), Emiyana Babweiga (65) na  Julliet Arshdes (40).

Kamanda wa polisi kikosi cha usalama barabarani nchini, Mohamed Mpinga amesema ni kweli ajali hiyo imetokea na kwamba majeruhi wapo katika hali nzuri.

 “Majeruhi walitibiwa na kisha kuendelea na safari hakuna aliyeumia sana,” amesema Mpinga

0 comments:

Post a Comment