CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema uhalifu unaoendelea kutokea wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani unatosha na kuitaka vyombo vya ulinzi na usalama kulichukulia suala hilo kwa uzito likome.
Kimesema yeyote mwenye dhamana na suala hilo ajitafakari kwani chama hicho kinahitaji watu wa maeneo hayo kurejeshewa imani na amani. Maeneo hayo yamekumbwa na mauaji mfululizo ya viongozi wa CCM. Katibu wa Sekretarieti, Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia suala hilo.
Alisema CCM imekuwa inafuatilia kinachoendelea katika maeneo hayo na kujiridhisha kuwa kuna haja ya Serikali na vyombo vya ulinzi kuongeza umahiri, ubunifu na weledi wa kushughulia uhalifu huo ili usiendelee. “Tunatoa rai kubwa kwa serikali, tumevumilia, tumekaa kimya na kufuatilia sana suala hili, Watanzania wanakufa, tunataka kuona kitu kinatokea chenye kurudisha amani na hata imani kwa wananchi,” alisema Polepole.
Alisema wananchi wa maeneo hayo wanaishi kwa hofu huku wengine wakikimbia nyumba zao ilhali ni haohao waliomchagua Rais John Magufuli, hivyo wana haki ya kuwa na maisha yenye amani kila siku. Alisema kama suala hilo ni ujambazi au ujangili inatosha na ifikie mwisho kwani hiyo ni moja ya namna nyingine kuhujumu wananchi na mali zao. Alisema vyombo vya ulinzi na usalama vishirikiane kurejesha amani, ili uchaguzi wa CCM unaotarajiwa kufanyika mwaka huu ufanyike salama.
“Kazi ya chama madhubuti ni kuwasemea watu, wapo waliouawa kikatili na watu wasio na mioyo, hisia wala utu wakati hakuna dini inayoamini katika kutoa uhai wa mtu isipokuwa Mungu pekee,” alisema Polepole. Alituma salamu za pole kwa wote walioathirika na uhalifu huo wakiwemo viongozi na wanachama wa chama hicho ambao wamepoteza uhai.
Friday, 26 May 2017
Home »
» CCM yajitosa uhalifu Kibiti
CCM yajitosa uhalifu Kibiti
Related Posts:
Chelsea: Diego Costa amesema klabu hiyo inataka kumuuza Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionCosta amesema angependa sana kurejea Atletico Madrid Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Diego Costa amesema amefahamishwa na meneja wa klabu hiyo Antonio Conte kwamba hayupo tena katika… Read More
Iringa: Majambazi wajeruhi na kupora fedha na dhahabu katika mgodi Kundi la watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevamia mgodi wa dhahabu wa wachimbaji wadogo katika kijiji cha Nyakavangala kilichopo katika tarafa ya Isimani wilayani Iringa na kupora fedha tasilimu kiasi cha zaidi ya shil… Read More
Man United kumtema Ibrahimovic Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionZlatan Ibrahimovic Timu ya Man united huenda isimuongeze mkataba mpya mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, mkataba wake wa sasa unamalizika Juni 30. Zlatan mwenye miaka 35 ali… Read More
Mkude: Kwa dau hili nipo tayari kujiunga na Yanga UNAWEZA ukashituka kidogo ila habari ndiyo hivyo anaweza kusaini Yanga kwa milioni 70 tu, Mkude ambaye mara kadhaa amewahi kuhusishwa kuwaniwa na Yanga ameamua kuweka wazi kuwa atatua ndani ya kikosi cha Yanga kwa ajili ya … Read More
Mkude: Kwa dau hili nipo tayari kujiunga na Yanga UNAWEZA ukashituka kidogo ila habari ndiyo hivyo anaweza kusaini Yanga kwa milioni 70 tu, Mkude ambaye mara kadhaa amewahi kuhusishwa kuwaniwa na Yanga ameamua kuweka wazi kuwa atatua ndani ya kikosi cha Yanga kwa ajili ya … Read More
0 comments:
Post a Comment