Wednesday, 24 May 2017

Wabunge Wakataa Kutoa Rambirambi Nyingine.

Mbunge wa Geita Vijini Joseph Msukuma (CCM) ameliomba Bunge kuazimia kutoa rambirambi kutokana na vifo vya watoto 10 vilivyotokea jimboni kwake vilivyosababishwa na mvua zilizonyesha mwishoni mwa wiki.

Ombi hilo limesababisha 'zogo' bungeni huku baadhi ya watunga sheria hao kusema hawatakubali kukatwa posho zao kwa kuwa rambirambi zimekuwa zikielekezwa kutekeleza miradi ya Serikali.

Katika hatua nyingine Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imepokea kwa huzuni na simanzi kubwa tukio la watoto 24 wanafunzi wa shule ya msingi kuzama majini na watatu kati yao kufa maji wakati wakitoka shuleni katika Kijiji cha Butwa, wilayani Geita.

0 comments:

Post a Comment