Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Kilimanjaro, Mzee Philemone Ndesamburo amefariki Dunia asubuhi ya leo katika Hospitali ya KCMC, Mkoani humo.
Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amethibitisha muda huu juu ya kifo hicho na kwamba bado haijafahamika chanzo cha kifo chake.
Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti hospitali ya rufaa ya KCMC.
Ndugu wakiwemo watoto wa marehemu wamefika Hospitalini hapo na kuomba mwili wa marehemu kufanyiwa uchunguzi kutokana na kifo kuwa ni cha ghafla.
Lema alisema, Mzee Ndesamburo alifika ofisini kwake majira ya asubuhi na alionekana mwenye afya njema, ilipofika majira ya saa nne hali ilibadilika na kushindwa kuendelea na majukumu yake.
Ndipo walipomkimbiza KCMC kwa ajili ya matibabu na alifariki dunia akiwa kitengo cha wagonjwa mahututi, Taarifa zaidi tutajulishana kadri zitakapokuwa zikitufikia.
SOURCE:MUUNGWANA
Wednesday, 31 May 2017
Home »
» BAADA YA KIFO:ndugu wataka uchunguzi kifo cha Ndesamburo
BAADA YA KIFO:ndugu wataka uchunguzi kifo cha Ndesamburo
Related Posts:
Fanya hivi kujichunguza kama una saratani ya matiti ( BREAST CANCER )Saratani ya matiti imekua ikiwatesa wanawake wengi kutokana na dalili zake kutoonekana mapema na pia wakati mwingine hali hii hutokea kwa sababu hawana tabia ya kuchunguza afya zao mara kwa mara na kupeleke kugundulika kua wa… Read More
Kaburi la baba wa Spika wa Bunge Job Ndugai lafukuliwa Wananchi wanafukua mabaki ya mwili wa baba wa Spika wa Bunge Job Ndugai, Yustino Ndugai aliyezikwa Bukombe ili kuyapeleka Kongwa. source:mwananchi … Read More
Fanya hivi pale mtoto mchanga anapopatwa na kwikwi. Kwikwi ni kitu cha kawaida kutokea hasa umri unavyozidi kwenda. Na mtoto mchanga yupo kwenye hatari zaidi ya kupata kwikwi, pia hata ndani ya mfuko wa kizazi kuanzia wiki ya sita mtoto huweza kupata kwikwi. Kwikwi hizi huwe… Read More
Umuhimu wa kufanya mazoezi ya kutembea Mazoezi ni muhimu kwa kila mmoja wetu, kwa sababu hayana uitaji wa gharama kubwa ukilinganisha na aina nyingine za mazoezi.Pia kutembea kwa kasi kwa muda wa saa moja na kuendelea imesadikika ya kwamba kuna faida zifuatazo;1… Read More
Wezi wavamia Nyumba, Wachinja kuku, wakapika, kula na kuosha vyombo Charity Njeri akionesha Masufuria yaliyutumika kupikia kuku Wezi wamevamia nyumba moja huko Kenya na kuchinja kuku, kupika, kula & kuosha vyombo kabla ya kutokomea na mali zenye thamani isiyojulikana. Kwamujibu w… Read More
0 comments:
Post a Comment