Muanzilishi wa mtandao wa kijamii Facebook, Mark Zuckerberg amerudi katika chuo kikuu cha Harvard University kutoa hotuba ya kuhitimu na kupokea shahada ya staha.
Zuckerbag ambaye ni mtu wa tano tajiri duniani,aliye na thamani ya $ bilioni 62.3, aliwacha masomo katikati kutoka chuo hicho cha Harvard baada ya kuuzindua mtandao huo wa kijamii duniani.
Amewataka wanaafunzi wasiunde "nafasi za aijira tu, bali wawe na malengo".
Wataalamu wa kisiasa wanadhani huenda anajitayarisha kuwania uongozi.
Katika hotuba yake Zuckerberg amewaambia wahitimu kwamba "tunaishi katika wakati ambao haujaimarika".
"Hizi ndio jitihada za wakati wetu, nguvu za uhuru , uwazi na jamii duniani dhidi ya nguvu za utawala wa kimabavu, kutengana na utaifa."
Mkewe akiwa mojawapo ya wageni , alinyoosha kidole kuelekea katika bweni alikokuwa akikaa wakati alipouzindua mtandao wa Facebook, na kutaja kwamba kukutana naye katika sehemu hiyo , ilikuwa ndio kitu bora alichopitia akiwa chuo kikuu.
Kabla ya kutoa hotuba hiyo, alipokea shahada ya staha ya sheria.
Zaidi ya watu bilioni 1.9 huingia Facebook kila siku.
Tangu kuzinduliwa kwake mnamo 2004, Facebook imezusha ushindani katika mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter, Snapchat na Instagram.
source:bbc
0 comments:
Post a Comment