Viongozi katika mkutano wa G7 wametofautiana kuhusu taarifa ya mabadiliko ya tabia nchi.
Viongozi sita walikubaliana kuunga mkono makubaliano ya mjini Paris ,ambayo ni ya kwanza yanayolenga kupunguza hewa chafu.
Hatahivyo Marekani imekataa kukubaliana ikisema kuwa itatoa uamuzi wake wiki ijayo.
Bwana Trump ambaye alidai kwamba ongezeko la joto duniani ni ''mzaha'' mara kwa mara ametishia kujiondoa katika makubaliano hayo.
Huu ni mkutano wa kwanza wa G7 kuhudhuriwa na Trump katika ziara yake ya kwanza ya kigeni.
Viongozi wa G7 kutoka Uingereza, Marekani ,Canada Ufaransa ,Ujerumani ,Italy na Japan wamekubaliana kuhusu kukabilina na ugaidi .
Kwa nini hakuna makubaliano kuhusu mabadiliko ya tabia nchi?
Tarifa ya mwisho iliotolewa katika mkutano huo unaofanyika nchini Itali ilisema kuwa Marekani iko katika harakati ya kufanyia marekebisho sera zake, hivyobasi kuhusu makubaliano ya Paris haitajiunga na mataifa mengine kukubaliana na swala hilo.
Hatahivyo mataifa hayo ya G7 yaliapa kuonyesha umoja wao katika kuidhinisha makubaliano hayo ya Paris.
Kansela wa Ujerumani alisema kuwa ''mazungumzo kuhusu mabadiliko ya tabia nchi hayaridhishi ,akiongezea kuwa kuna hali ya mataifa sita dhidi ya ya taifa moja''.
0 comments:
Post a Comment