Friday, 26 May 2017

Ngozi ya Samaki kutibu majeraha ya moto

Madaktari wa Brazil wameanza kutumia ngozi ya samaki aina ya Tilapia kutibu majeraha ya moto wakisema ngozi ya aina hiyo ya samaki ina kiwango kikubwa cha madini ya collagen na protein ambayo husaidia majeraha makubwa ya moto kupona haraka.

Wanasayansi hao wameanza rasmi kutumia njia hiyo inayodaiwa kuwa na ufanisi mkubwa zaidi ya kutumia bendeji za kawaida kwa kuwa ngozi ya Samaki hao inasaidia kupambana na maambukizi ya bakteria wanaoshambulia majeraha ya moto ikiwa na madini yanayosaidia kufuta alama za kuungua kwa haraka.

Inaelezwa mpaka sasa zaidi ya wagonjwa 56 waliotibiwa kwa kutumia ngozi ya Samaki hao wameonesha maendeleo mazuri. Kwa mujibu wa madaktari hao ngozi ya Nguruwe pia inaweza kutumika kufungia vidonda vinavyotokana na moto kutokana na kiwango kikubwa cha collage iliyopo kwenye ngozi hiyo

Related Posts:

  • Mtaji wa Soko la Hisa DSM waporomoka Ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) umepungua kwa Shilingi Bilioni 380 kutoka Shilingi Trilioni 20.2 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 19.9 kwa wiki iliyoishia Mei 19 mw… Read More
  • Mwanamke wa India aweka rekodi ya kuupanda Mlima Everest Mwanamke mzaliwa wa India amefanikiwa kuupanda Mlima Everest hadi kileleni katika kipindi cha chini ya wiki moja ambayo huenda ikawa rekodi mpya kwa wanawake. Anshu Jamsenpa, 37, ambaye ni mama wa watoto wawili, alifika ki… Read More
  • Vijana wanne wambaka binti wa miaka 15 Watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi huku mwingine mmoja akiendelea kutafutwa kwa tuhuma za kumbaka binti mmoja mwenye umri wa miaka 15 wilayani Ilemela, mkoani Mwanza.Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mw… Read More
  • Nyumba zateketea kwa moto Sengerema Sengerema. Nyumba za wavuvi ambazo idadi yake haijajulikana hadi sasa katika kisiwa cha uvuvi cha Nyamango Kata ya Bulyaheke  halmashauri ya Buchosa wilayani hapa, zinateketea kwa moto ambapo chanzo chake hakijajul… Read More
  • Mbunge atinga bungeni na rundo la risiti Dodoma.Mbunge wa Viti maalum (Chadema), Rhoda Kunchela aliwasilisha bungeni furushi la risiti za mwenge wanazodaiwa kuchangishwa kwa nguvu, walimu na wafanyabiashara.Mbunge Kunchela aliomba kutoa hoja ili ijadiliwa na Bunge … Read More

0 comments:

Post a Comment