WAFANYAKAZI wanne wa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kufanya upasuaji kwenye mwili wa maiti na kuchukua madawa ya kulevya kisha kuyauza madawa hayo.
Akizungumza na wanahabari mapema leo (Mei 26, 2017), Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro amesema;
“Yule Mghana aliyekutwa amefariki dunia Machi 14, 2017 katika nyumba ya kulala wageni inayoitwa Red Carpet iliyopo Sinza, alichukuliwa kupelekwa Mwananyamala Mochwari (chumba cha kuhifadhia maiti), lakini wale wafanyakazi wa kwenye ile mochwari nafikiri walipata taarifa kuwa mwili ule una madawa ya kulevya, hivyo walifanya njama wakapasua ule mwili na kutoa kete 32 za madawa ya kulevya ambayo kimsingi waliyauza.
“Baada ya jeshi la polisi kuwahoji wamekiri kwamba ni kweli walihusika kuupasua mwili huo na kuchukua kete za madawa, baada ya hapo waliyauza madawa na huyo waliyemuuzia tumekwishamkamata.
Sirro alienda mbele zaidi na kueleza;
“Huyo aliyeuziwa naye alikwenda kumuuzia jamaa mmoja anayeitwa Ally Nyundo ambaye yumo kwenye orodha ya wauza madawa waliotajwa na Mkuu wa Mkoa, na tulishawahi kumpeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali akabainika anatumia madawa ya kulevya.
“Kwa hiyo mpaka sasa tunawashikilia watuhumiwa watano wa tukio hilo ambapo wanne ni wahudumu wa hiyo mochwari na mmoja ni yule waliyemuuzia kete hizo za madawa, hivyo tunaandaa jarada kwa ajili ya kulipeleka kwa wakili wa serikali” alisema Sirro.
Friday, 26 May 2017
Home »
» Baada ya Kupasua Maiti na Kuchukua Kete za Madawa, Wafanyakazi wa Mochwari watiwa Mbaroni
Baada ya Kupasua Maiti na Kuchukua Kete za Madawa, Wafanyakazi wa Mochwari watiwa Mbaroni
Related Posts:
Tanzania’s new governor says appointment took him by surprise Newly appointed Bank of Tanzania (BoT) governor Florens Luoga Dar es Salaam. Newly appointed Bank of Tanzania (BoT) governor Florens Luoga has said he was taken by surprise over President John Magufuli’s announc… Read More
Magufuli atema cheche wakati akifungua barabara KIA-MIRERANI Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli ameshatua uwanja wa ndege wa Kilimanjaro na kupokelewa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Mama Anna Elisha Mngwira. Muda mchache ujao anatarajiwa kuzindua barabara ya K… Read More
Nyalandu Kumpeleka Tundu Lissu Marekani Kwa Matibabu Zaidi.Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu, amesema anasubiri ripoti ya madktari wa Agha Kan Nairobi, ili kuweza kuchukua hatua zaidi za kumhamishia Marekani Tundu Lissu kwa matibabu zaidi. … Read More
Russia test-launches 4 ballistic missiles from submarines and space centre Russia launched four ballistic missiles on Thursday (26 October) as part of large-scale war games involving the country's strategic forces, the country's defence ministry said in a statement. Three of the projectiles were fir… Read More
This is what Zarizebosslady said today after Diamond confessing to cheat her.Am such an early morning person as some can see on my snap, usually up by 5am. Let's start this day on a different note, shall we. Ladies and gentlemen I've heard you loud and clear, the advises, the consolation, the pity, th… Read More
0 comments:
Post a Comment