Viongozi wa eneo la mashariki nchini Kenya wameonya kwamba maeneo ya taifa hilo huenda yakanyakuliwa na wapiganaji wa Al-Shabab.
Gavana wa kaunti ya Wajir ambayo inapakana na taifa la Somalia amesema maswala ya mauaji ya machifu wa eneo hilo, mabomu ya kutegwa barabarani, pamoja na uharibifi wa vifaa vya mawasiliano hayapewi umuhimu mkubwa.
Gavana wa kaunti ya Mandera, Ali Roba ambaye msafara wake ulishambuliwa na wapiganaji wa Al-Shabab amesema kuwa serikali kuu inahitaji kuingilia swala hilo kwa haraka.
Kundi la wapiganaji wa Al-Shabab linadhibiti maeneo mengi nchini Somalia na linawaajiri wapiganaji kutoka Kenya na mataifa mengi ya Afrika mashariki.
0 comments:
Post a Comment