Wednesday, 31 May 2017

Mbunifu wa Android azindua simu mpya ya Essential

Essential PhoneHaki miliki ya pichaESSENTIAL PHONE
Image captionSinu ya Essential hutumia mfumo wa Android na imeanza kuuzwa nchini Marekani kwa dola $699.
Andy Rubin, ambaye ni miongoni mwa watu waliobuni programu ya software Android ya Google, amezindua simu yake ya smartphone yenye ncha ndefu.
Bwana Rubin aliacha kazi katika Google mwaka 2014 kwa ajili ya kubuni kampuni yake ya uwekezaji wa kiteknolojia.
Essential ni moja wapo ya kampuni zinazodhaminiwa na kampuni ya Rubin - na simu ya Essential ni moja ya bidhaa zake.
Simu hiyo hutumia mfumo wa Android na imeanza kuuzwa nchini Marekani kwa dola $699.
Hata hivyo, itakuwa ni vigumu kwa kampuni hiyo kujipenyeza katika masoko makubwa ya ambayo tayari yameimarisha mauzo ya bidhaa zake nchini humo.
Samsung kwa sasa ndio yenye soko kubwa la hisa katika soko la simu za Smart, ikiwa na mauzo ya asilimia 21% kote duniani, kulingana na mchambuzi wa masuala ya makampuni Gartner. Apple ina soko la asilimia 14%.
simu ya EssentialHaki miliki ya pichaESSENTIAL PHONE
Image captionKioo cha simu ya Essential kimefunika karibu uso wote wa simu
Licha ya makampuni makubwa ya Uchina yanayouza simu zenye gharama ya chini, viwanda vidogo vidogo vimepata ugumu wa kupata walau asilimia moja ya hisa kwenye soko za bidhaa zao  na bei ya simu ya Essential inaiweka kwenye hali ya changamoto kubwa zaidi
Lakini Bwana Rubin aliiambia hadhira ya watu mjini California kwamba anaamini kuna nafasi ya soko la Android kwa muuzaji mwingine licha ya Samsung, na kwamba Essential inalenga kuwa kampuni kuu inayotoa aina mbali mbali za bidhaa kwa mnunuzi
Essential phone imetengenezwa kwa madini ya titanium na ina kioo kilichoenea sehemu kubwa ya simu na sehemu isiyo na kioo ni ndogo zaidi.

Related Posts:

  • Hatimaye simu mpya za Nokia 3310 zaingia madukani  Simu hizo mpya za Nokia 3310 zitakaa muda mrefu na chaji kuliko simu asiliSimu za Nokia 3310 zimeanza kuuzwa tena madukani, takriban miaka 17 baada ya simu hizo kuanza kuuzwa mara ya kwanza.Simu za sasa zina kamera ya… Read More
  • CCM yajitosa uhalifu Kibiti CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema uhalifu unaoendelea kutokea wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani unatosha na kuitaka vyombo vya ulinzi na usalama kulichukulia suala hilo kwa uzito likome.Kimesema yeyote mwen… Read More
  • Neema Ajira zaidi za 250 Wizara ya Ardhi SERIKALI imezidi kutangaza neema ya ajira kwa Watanzania baada ya kubainisha kuwa katika mwaka ujao wa fedha watumishi wapya 291 wataajiriwa katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Waziri wa wizara hiyo… Read More
  • Dola ya Marekani inateteleka WATUNGA sera kutoka Benki Kuu ya Marekani, wamesema wanafuatilia kilichoko katika uchumi wa taifa, kutokana na kuongezeka kiwango cha riba za benki nchini humo na imefanya thamani ya fedha za dola kushuka.Mchumi wa nchi hiy… Read More
  • Aua mkewe kisa pesa ya matibabu JESHI la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia Pastory Chilangazi (37), mkazi wa Kijiji cha Mamvisi, Wilaya ya Gairo kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kipigo kutokana na kile kinachoelezwa ni kutofautiana baada ya mkewe huyo ku… Read More

0 comments:

Post a Comment