Wednesday, 24 May 2017

Polisi 4 wauawa katika mlipuko Garissa Kenya

Maafisa wa usalama GarissaHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMaafisa wa usalama katika shambulio la 2015 ambapo watu 147 waliuawa katika shambulio la al Shabaab dhidi ya chuo kikuu cha Garissa Kenya
Maafisa 4 wa polisi wameuawa na wengine 4 kujeruhiwa, mmoja akiwa katika hali mahututi, katika shambulio Jumatano alfajiri eneo la Liboi kaskazini mashariki mwa Kenya karibu na mpaka na Somalia.
Duru za usalama zinaarifu kuwa gari la kijeshi lililokuwa limewabeba maafisa wa usalama wa Kenya lilikanyaga bomu la kutegwa ardhini.
Taarifa katika baadhi ya vyombo vya habari Kenya zinasema kuwa maafisa hao walikuwa wanapiga doria katika eneo la Kulan wakati gari lao lilipokanyaga bomu hilo.
Maafisa wengine watatu wamejeruhiwa katika shambulio hilo na inaarifiwa wamesafirishwa hadi mjini Nairobi kupokea matibabu maalum.
Awali katika mtandao wa kijamii Twitter - Shirika la msalaba mwekundu limesema: " gari limekanyaga bomu la ardhini na kuwajeruhi watu 8 baina ya Liboi na Kulan, kaunti ya Garissa."Liliendelea kusema kwamba linashughulikia tukio hilo.
Gazeti la Daily Nation linaripoti kuwa maafisa hao walikuwa wanasafiri kwa gari la kituo cha polisi cha Kulan katika barabara ya Liboi - Milan wakati gari hilo lilipokanyaga bomu la kutegwa ardhini.
Inaarifiwa gari hilo liliharibika vibaya.
Makamu wa rais William Ruto ametuma ujumbe katika Twitter akisema, "Waathiriwa wa shambulio la Liboi kaunti ya Garissa wamo mawazoni mwangu. Ni lazima tuujenga ukuta mpakani".
Serikali ya Kenya iliidhinisha ujenzi wa ukuta katika mpaka baina ya Kenya na Somalia kuzuia uhalifu baada ya shambulio la kigaidi dhidi ya chuo kikuu cha Garissa mnamo mwaka 2015.

SOURCE:BBC

Related Posts:

  • Pogba kutua Tanzania Klabu ya Everton inajiandaa kuja nchini Tanzania kwa ziara ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi ambapo wakiwa hapa wtacheza na washindi wa kombe la Sports Pesa timu ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya. Sasa Everton wanaweza … Read More
  • Hawa wote motoni KIMENUKA! RAIS John Magufuli ameagiza kukamatwa na kuhojiwa kwa waliokuwa mawaziri, kamishina wa madini, wanasheria wakuu (AG) na waliokuwa watumishi katika idara mbalimbali za serikali zilizoruhusu usafirishaji wa madini … Read More
  • Diamond afunguka mchango wa Wema Sepetu kwenye ‘Chibu Perfume’. Msanii wa muziki, Diamond platnumz amefunguka kuuzungumzia mchango wa malkia wa filamu, Wema Sepetu kwenye perfume yake ya ‘Chibu Perfume’.Diamond amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa, yeye na Wema wanakutana na ku… Read More
  • Serikali imezuia Passport za Chenge, Muhongo, Kafumu, Karamagi Serikali imeagiza, Mawaziri, Wanasheria Wakuu wa Serikali na Manaibu wao, Wakurugenzi wa idara za mikataba, na Makamishna wa madini, wanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini na watumishi wengine wa Serikali na watu wote wa… Read More
  • Wananchi watema cheche, wataka Marais wastaafu wachunguzwe Mikoani. Wananchi katika maeneo mbalimbali nchini wamemshauri Rais John Magufuli kufanya mabadiliko ya Katiba na kuhakikisha diplomasia ya uchumi haivurugiki kutokana na sakata la mchanga wa madini (makinikia).Wakitoa maoni… Read More

0 comments:

Post a Comment