Monday, 5 June 2017

Mti mrefu barani Afrika uko Tanzania,ni kivutio watalii

Tanzania
Image captionDk. Andreas Hemps akiupima mti huo mrefu barani Afrika aina ya Mkukusu
Mkoa wa Kilimanjaro uliopo kaskazini mwa Tanzania, ni maarufu kwa shughuli za utalii.
Kila mwaka watalii huja kwa lengo la kupanda Mlima Kilimanjaro. Lakini hivi sasa, watalii wamepata kivutio chengine mkoani humo.
Hii ni baada ya serikali ya Tanzania kutangaza kuwepo kwa mti mrefu zaidi barani Afrika. Mti huu aina ya Mkukusu una urefu wa mita 81.5 na unaopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA).
Ni matokeo ya utafiti uliofanywa na Dk. Andreas Hemps na mkewe wote kutoka nchini Ujerumani ndio waliobaini kuwepo kwa mti huo umbali wa mita 1600 kutoka usawa wa bahari baada ya utafiti uliohusisha nchi nyengine barani Afrika kwa kipindi cha miaka mitano.
"Nimefika hapa ilikuwa Krismasi mwaka 1996 na nimeingia kufanya utafiti wa msitu. Nimeona miti hii na kusema hii ni kitu kikubwa lakini nilikuwa sijajua kama ni mita 80. Natumia leza skana. Napima mara tatu halafu ndio napata urefu kamili. Wageni wengi watafika hapo kushuhudia mti huu, pamoja na watafiti vilevile. Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro pia nayo imeanza kuangalia mazingira haya ili yasiharibiwe," Dk. Andreas Hemps amemweleza mwandishi wa BBC Aboubakar Famau.
Licha ya mti huu kuwa kivutio ambacho kinaweza kuiingizia serikali fedha za kigeni, lakini changamoto iliopo ni ugumu wa kuufikia mti huo.
Ili kufika katika eneo la Mrusungu ambapo ndipo ulipo mti huo mrefu zaidi, ni safari ya kutembea kwa mguu kwa takriban muda wa saa nne kwenda na kurudi kwa kupita katika milima, mabonde, mito na makorongo.
Kazi iliyofanywa na watafiti hao, inaonekana kuupa heshima mkoa wa Kilimanjaro na Tanzania kwa jumla na mti huo utaongeza chachu ya watalii kupanda Mlima Kilimanjaro na wengine kwenda kushuhudia mti huo.
Tanzania
Image captionCharles Ngendo ambae ni mhifadhi wa utalii katika Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro
Kwa upande wake, Charles Ngendo ambae ni mhifadhi wa utalii katika Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro amesema hifadhi inatarajia kuboresha miundombinu ya kufika katika mti huo ili kuwawezesha watalii kwenda kwani miundombinu ya sasa hivi sio rafiki kwa utalii.
"Niseme tu kwamba Kinapa tutaweka mikakati ya kuhakikisha kwamba eneo hili linaendelezwa ili liwe sehemu ya utalii katika hifadhi ya taifa ya Kilimanjaro. Tutaweka katika bajeti zetu za hifadhi kuhakikisha kwamba tunaboresha miundombinu. Kama unavyoona mahala hapo kuna makorongo, kuna miinuko. Na ili paweze kufikika lazima kuwe na miundombinu. Kwa mfano tutaweza madaraja baadhi ya maeneo," ameeleza Charles Ngendo.
Tanzania
Image captionCharles Ngendo mhifadhi KINAPA (kulia), Dk Andreas Hemps (wapili kulia ), katikati mwandishi wa BBC Aboubakar Famau
Mti huo wenye umri wa zaidi ya miaka 600 hivi sasa uko chini ya ulinzi wa KINAPA ili kuulinda kutokana na majangili na hata wale wanaotaka kuutumia kama dawa. Mti huo tayari umeingizwa katika rekodi ya dunia kwa kushika nafasi ya sita kwa urefu duniani.
Utafiti wa kuwepo kwa mti huo tayari umewekwa katika mitandao na vituo vya utalii katika nchi mbalimbali duniani, ili kuleta changamoto ya utafiti mwengine utakaoweza kuonesha mti mwengine mrefu katika nchi nyengine yoyote Barani Afrika.

Related Posts:

  • Everton kumsajili PickfordHaki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionKipa wa Sunderland Jordan Pickford Klabu ya soka ya Everton imefikia makubaliano ya kumsajili kipa Jordan Pickford kutoka klabu ya Sunderland kwa dau pauni milioni 30. Pickford, k… Read More
  • Ronaldo kushtakiwa kwa kukwepa kodi Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionChristiano Ronaldo akicheza fainali za Champion League Mamlaka nchini Uhispania zitamfungulia mashtaka nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, akishutumiwa kwa kukwepa kul… Read More
  • Hawa wote motoni KIMENUKA! RAIS John Magufuli ameagiza kukamatwa na kuhojiwa kwa waliokuwa mawaziri, kamishina wa madini, wanasheria wakuu (AG) na waliokuwa watumishi katika idara mbalimbali za serikali zilizoruhusu usafirishaji wa madini … Read More
  • Korea Kaskazini yamwachilia huru MmarekaniHaki miliki ya pichaREUTERSImage captionWazazi wa Otto Warmbier waliohifia usalama wa mwana wao kufuatia kuongezeka kwa uhsama kati ya Marekani na Korea Kaskazini Korea Kaskazini imemwachilia huru mwanafunzi Mmarekani Otto Wa… Read More
  • Mwanamke ajichinja kwa chupa MWANAMKE aliyefahamika kwa jina la Saada Elias (24) mkazi wa Mtaa wa Mabambase katika Manispaa ya Shinyanga alifariki dunia kwa kujikata koromeo kwa chupa ya soda. Mwanamke huyo alijiua kwa chupa ikiwa ni muda mfupi baa… Read More

0 comments:

Post a Comment