Jeshi la Polisi Mwanza linawashikilia watu wanne baada ya kuwakuta na dawa za kulevya aina ya Mirungi mafungu 57 yenye ukubwa wa kilogramu 56.75 ambayo yalikuwa yamewekwa kwenye mabegi na magunia.
Kamanda wa Polisi Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuwa polisi waliwakamata watuhumiwa hao leo majira ya saa kumi na moja alfajiri katika mtaa wa Mbugani 'A' Kata ya Mbugani wilayani Nyamagana.
"Askari wakiwa kwenye doria na misako walifanikiwa kuwakamata watu wa nne waliofahamika kwa majina ya Thomas Zacharia (25), mkazi wa mtaa wa Unguja Mwanza, Ally Athumani (35) mkazi wa Kahama Shinyanga, Nyamurya Elia (35) mkazi wa mtaa wa Unguja Mwanza, na Stanslaus Mapinduzi Elias (41) mkazi wa Tarime, wakiwa na dawa za kulevya aina ya mirungi mafungu 57, yenye kiasi cha kilogramu 56.75, yakiwa yamemewekwa kwenye mabegi na magunia, kitendo ambacho ni kosa la jinai" ilisema taarifa ya Msangi
Kufuatia sakata hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Naibu Kamishina wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wakazi wa jiji na mkoa wa Mwanza hususani vijana akiwataka kuacha kujihusisha na biashara za madawa kwani ni kosa kisheria.
Wednesday, 7 June 2017
Home »
» Wakamatwa na dawa za kulevya Mwanza
Wakamatwa na dawa za kulevya Mwanza
Related Posts:
Rais wa FIFA aipongeza Yanga Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, Mei 24, mwaka huu alituma ujumbe Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuipongeza Young Africans ya Dar es Salaam kwa kutwaa ubingwa Ligi Kuu… Read More
HIZI HAPA NAMBA ZA MAMENEJA WA TANESCO KILA WILAYA TANZANIASASA UNAWEZA KUWASILISHA KERO ZAKO MOJA KWA MOJA AU KUWASILIANA NA MAMENEJA WA TANESCO WILAYA KUPITIA NAMBA ZIFUATAZO HAPO CHINI. BONYEZA HAPA>>>>>>>NAMBA ZA SIMU ZA MAMENEJA WA TANESCO KILA WILAYA… Read More
Prof. Maghembe ataka walionyang’anywa pikipiki warudishiwe Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe akijibu hoja mbalimbali za Wabunge waliochangia bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018. Serikali imeagiza kurejeshwa mara moja kwa pikipiki, baiskel… Read More
TAMBUA VYUO VINAVYOTAMBULIKA NA NACTENIMEAMUA KUKUWEKEA ORODHA YA VYUO VINAVYOTAMBULIKA NA NACTE ILI KUEPUKA KUTAPELIWA NA VYUO FEKI. BONYEZA HAPA>>>>>>>>.ORODHA YA VYUO VINAVYOTAMBULIKA NA NACTE… Read More
Wanafunzi 33 Meatu wamekatisha masomo kutokana na Ujauzito Mimba imekuwa ni chanzo kimojawapo kinachochangia kurudisha nyuma ustawi wa elimu hapa nchini. Wanafunzi 33 wa sekondari wilayani Meatu mkoani Simiyu wamekatisha masomo yao baada ya kupata ujauzito katika kipindi cha mw… Read More
0 comments:
Post a Comment