Tuesday, 13 June 2017

Serikali imezuia Passport za Chenge, Muhongo, Kafumu, Karamagi

Serikali imeagiza, Mawaziri, Wanasheria Wakuu wa Serikali na Manaibu wao, Wakurugenzi wa idara za mikataba, na Makamishna wa madini, wanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini na watumishi wengine wa Serikali na watu wote waliohusika katika kuingia mikataba ya uchimbaji madini, utoaji wa leseni za uchimbaji wa madini na kuongeza muda wa leseni, watumishi na wamiliki wa makampuni ya madini kuto toka nje ya mipaka ya Tanzania.

Agizo hilo lilitolewa jana  na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ambaye alisema kuwa, wote waliotajwa kuhusika katika kulisababishia taifa hasara kupitia sekta ya madini, hawaruhusiwi kutoka nje ya mipaka ya Tanzania isipokuwa kwa kibali maalum kutoka serikalini.

“Naelekeza wote waliotajwa kuhusika hakuna kutoka nje ya mipaka ya nchi yetu isipokuwa kwa kibali maalum kutoka serikalini. Vyombo vitekeleze maagizo ya Rais kwa utimamu,” aliandika Waziri Nchemba kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Agizo hili limekuja ikiwa ni saa chache tangu Rais Magufuli alipoagiza kuwa, viongozi wote na watumishi mbalimbali waliohusika katika kusaini mikataba mibovu na kushiriki kwa namna yoyote ile, wahojiwe.

Miongoni mwa watakaoathiriwa na zuio hilo, ni pamoja na Maafisa wa TRA, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Andrew Chenge, Mwanyika, na Werema, Mkurugenzi Idara ya Mikataba, Mary Ndosi, Kamishna Dalali Peter Kafumu, Waziri Prof. Muhongo, Waziri Daniel Yona, Waziri Nazir Karamagi, Jaji Julius Malaba, Waziri William Ngeleja.

Awali Waziri Nchemba alimpongeza Rais Magufuli kwa jitihada alizozichukua katika kuhakikisha analinda rasilimali za wanyonge na kusema kuwa hakuna uzalendo kama huo.

“Hakuna uzalendo zaidi ya kulinda rasilimali za Taifa, Hakuna utetezi wa wanyonge zaidi ya kulinda rasilimali zao.Hongera sana Mh.Rais kwa uzalendo wa vitendo kwa Taifa letu.”

source:muungwana

Related Posts:

  • Mgombea urais adaiwa kutaka kujirusha kutoka kwenye ghorofa KenyaImage captionRaia wakijisajili kuwa wapiga kura nchini Kenya awali. Uchaguzi mkuu utafanyika Agosti 8 Mmoja wa waliojitokeza kugombea urais katika uchaguzi mkuu mwezi Agosti nchini Kenya alijaribu kujirusha kutoka jumba la gh… Read More
  • Ikulu yatoa majibu haya kwa Acacia Dar es Salaam. Uamuzi wa Serikali kuhusu suala la usafirishaji wa mchanga wa madini, utategemea ripoti ya kamati ya pili iliyoundwa na Rais John Magufuli kuchunguza suala hilo.Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi wa M… Read More
  • Watu watatu wafa na mmoja kanusurika Rufiji Rufiji. Watu watatu  wamefariki dunia kwa kuzama majini na mmoja kunusurika kifo baada ya mtumbwi waliokuwa wakivukia kuzama bwawani wilayani Rufiji mkoani Pwani.Akithibitisha kutokea kwa vifo hivyo, Ofisa Tarafa … Read More
  • Askofu Gwajima: nitawavua mataulo wanaonichokoza Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amewatahadharisha wanaomchokoza akisema ni sawa na mtu anayeanzisha ugomvi huku akiwa amevaa taulo.Akihubiri leo, Gwajima amesema wakiendelea atawavu… Read More
  • Mgeja akasirishwa na kauli ya Polepole Morogoro. Mwenyekiti wa Tanzania Mzalendo Foundation, Khamis Mgeja amemuonya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hampyrey Polepole aache mara moja kugeuza matukio ya kuuawa Watanzania katika Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani… Read More

0 comments:

Post a Comment