Wednesday 14 June 2017

Aliyekuwa gavana wa Rio de Janeiro afungwa miaka 14 kwa ufisadi

Rio de Janeiro's Governor Sergio Cabral smiles as he visits the site of the construction of a new tunnel to the Transolimpica expressway in Rio de Janeiro, Brazil, on November 08, 2013.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSergio Cabral alihudumu mihula miwili kama gavana wa Rio kuanzia mwaka 2007 hadi 2014.
Aliyekuwa gavana wa jimbo la Rio de Janeiro nchini Brazil, amehukumiwa kifungo cha miaka 14 gerezani kwa ufisadi na ulanguzi wa pesa.
Sergio Cabral alihudumu mihula miwili kama gavana wa Rio kuanzia mwaka 2007 hadi 2014.
Analaumiwa kwa kupokea hongo kutoka kwa makampuni ya ujenza ili kuyapa zabuni za pesa nyingi.
Jaji Sergio Moro, alisema kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kumshtaki mkewe, Adriana Ancelmo
Cabral alikamatwa mwezi Novemba kama sehemu ya oparesheni iliyofahamka kama Car Wash, iliyohusu uchunguzi mkubwa, ambayo ilisababisha kukamatwa kwa wanasiasa mashuhuri na wafanyibiashara nchini Brazil.
Cabral ni mwanachama wa cham cha Democratic Movement Party, cha rais Michel Temer ambaye pia anafanyiw uchunguzi unaohusu ufisadi.
Jaji Moro alisema kuwa gavana huyo wa zamani alikuwa amechukua dola 813,000.
Hata hivyo jaji amesema kuwa pesa hizo hazijapatikana na huenda Cabral alizihamisha kabla ya akaunti zake kufungwa.

0 comments:

Post a Comment