Wednesday, 14 June 2017

Mbowe atema nyongo

Siku moja baada ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Galasius Byakanwa kuongoza uondoaji wa miundombinu katika shamba la Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, mwenyekiti huyo ameandika hivi ivi katika ukurasa wake wa Instagram:

"Najua haya yanatokea kwa sababu ya misimamo yangu ya kisiasa kwa sababu wa muelekeo wangu wa kisiasa na uthabiti na uimara wa chama ninachokiongoza, sasa mimi siwezi kuwa kondoo, nimesema siku zote, haya mambo ya duniani anayeyalipa ni Mungu, si mtawala yeyote yule.

“Hawatabadilisha mawazo yangu kwa kuharibu mali zangu, wanaweza kuharibu zote hata wakitaka roho yangu waichukue, waichukue tu lakini haitanisababisha nibadili msimamo wangu katika kuamini ninachokisimamia, ninachokipigania katika Taifa."

"Hakuna wingi wa mali ambao wataharibu utakaonifanya Mbowe nikapige magoti kama wengine wanavyopiga magoti, sitapiga magoti, nitasimama katika kweli na haki wakati wote wa maisha yangu, kwa hiyo hili halinishangazi kwa sababu najua gharama ya ninachokilipa.

“Wako watu wengi wamenipigia simu wakijaribu kunipa pole kunitia moyo, wengine wamejaribu kunitia hofu, wakiniambia Mwenyekiti Mbowe pengine uachane na siasa, nimewaambia sitoachana na siasa, nitafanya siasa, ilimradi ni siasa safi zenye kusimamia ukweli na haki nitasimama nazo."

Miundombinu ya shamba hilo iliharibiwa kwa kinachoelezwa kuwa lipo karibu na chanzo cha ma

Related Posts:

  • AJUCO THIRD YEAR WATUNISHIWA MISULI NA RMA Katika kile ambacho hakikutarajiwa na mashabiki wengi wa AJUCO third year lakini kimewezekana ni baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya timu ya chuo cha wauguzi Songea maarufu kama RMA. Mechi hiyo ilichezwa katika… Read More
  • Mwanamke ajioa baada ya kukosa mchumba Q May Chen Anasema kwamba ameamua kuafikia ndoto yake kupitia kupiga picha za harusi. Alijichagulia marinda yote manne na vito alivyovaa Mwanamke mmoja ambaye anaugua saratani ya matiti amejioa mwenyewe baada ya kusubiri mc… Read More
  • Trump amuonya mkuu wa FBI aliyefutwa James Comey Rais wa Marekani Donald Trump amemtahadharisha mkuu wa shirika la uchunguzi wa jinai FBI aliyefutwa kazi James Comey dhidi ya kufichua habari kwa vyombo vya habari. Bw Trump ameandika kwenye Twitter kwamba Bw Comey heri "a… Read More
  • Jambazi wa kike auawa na polisi Nairobi Mwanamke anayedaiwa kuwa jambazi sugu, ambaye amekuwa akipakia mtandaoni picha zake akiwa amejipodoa na kujipamba, ameuawa na polisi jijini Nairobi. Kijana huyo ambaye ametambuliwa kama Claire Mwaniki aliuawa na polisi alf… Read More
  • MWAKA WA TATU WAKUBALI KIPIGO TENAIkiwa ni mwendelezo wa michuano ya AJUCO ligi (inter class), leo hii majira ya jioni hali imekuwa mbaya kwa wakongwe wa chuo cha AJUCO (third year) baada ya kukubali kipigo cha magoli 3-2 kutoka kwa wadogo zao mwaka wa kwanza… Read More

0 comments:

Post a Comment