AKILIMALI
Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahimu Akilimali ametangaza kuwania nafasi ya uenyekiti wa klabu ya hiyo iliyoachwa wazi hivi karibuni na aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji.
Hivi karibuni Manji alitangaza kujiuzulu kwenye nafasi yake hiyo ili aweze kupumzika kutokana na matatizo mbalimbali aliyokumbana nayo siku chache zilizopotia.
Lakini pia maamuzi hayo ya Manji yalikuja ikiwa ni muda mfupi tu umepita tangu alipotangaza kutaka kuikodi timu hiyo kwa muda wa miaka 10, lakini akakukumbana na changamoto kibao kutoka kwa baadhi ya wanachama wa klabu hiyo na kuamua kusitisha mpango wake huo.
Akilimali alisema anaamini amefikia uamuzi huo ili aweze kuleta mabadiliko makubwa ya ndani ya klabu hiyo kuanzia pale Manji alipoishia.
Alisema licha ya kutokuwa bilionea kama ilivyokuwa kwa Manji lakini anaamini kwa kutumia utajiri wake wa hekima na busara alizonazo ataiongoza klabu hiyo kwa mafanikio makubwa, kwa hiyo amewataka wanachama kutulia.
“Manji keshaondoka Yanga akapumzike kutokana na matatizo yaliyompata hivi karibuni kwa hiyo siyo vizuri kuanza kuumiza vichwa kuwa mambo yatakuaje bila ya yeye.
“Yanga ni timu kubwa, jina lake na nembo yake tu chanzo kikubwa cha kuingizia mapato endapo atapatikana kiongozi mwenye uchungu na maendeleo ya Yanga na asiwe mpigaji.
“Kwa hiyo, katika uchaguzi ujao ambao utafanyika ili kuziba nafasi iliyoachwa na Manji, nitagombea nafasi hiyo kwani uwezo wa kuipa Yanga mafanikio ninao,” alisema Akilimali.
0 comments:
Post a Comment