Wednesday 14 June 2017

TAMBUA:Aspirin ni hatari kwa watu wenye umri mkubwa

Vidonge vya Aspirin ni hatari kwa watumiaji wa umri wa zaidi ya miaka 75Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionVidonge vya Aspirin ni hatari kwa watumiaji wa umri wa zaidi ya miaka 75
Watu walio na umri wa zaidi ya miaka 75 ambao hutumia dawa aina ya Aspirin baada ya kupata kiharusi au maradhi ya moyo wako hatarini kupata matatizo ya kuvuja damu tumboni,Shirika la utafiti wa kitabibu Lancet limeeleza.
Wanasayansi wanasema, kupunguza athari hizo , watu walio na umri mkubwa wanapaswa kumeza dawa za kuzuia maradhi ya tumboni (PPI)
Lakini wamesisitiza kuwa Aspirin ina faida muhimu kama vile kuzuia maradhi ya moyo
Utafiti wa kitabibu nchini Uingereza umeashiria kwamba kumeza vidonge vya dawa aina ya Aspirin kuna athari kubwa zaidi kuliko ilivyodhaniwa hapo awali hususan kwa watu wenye umri mkubwa. Dawa hiyo ambayo inatumiwa sana kuzuia mshtuko wa moyo na maradhi ya kiharusi imehusishwa kwa siku nyingi kusababisha matatizo ya uvujaji wa damu ndani ya tumbo.
Wataalam hao wametahadharisha kuwa kusitisha ghafla matumizi ya Aspirin kunaweza kuleta madhara, hivyo mtu yeyote anashauriwa kupata ushauri wa Daktari ikiwa anatakiwa kubadili dawa.

0 comments:

Post a Comment