Mwanafunzi raia wa Marekani ambaye aliachiliwa kutoka gerezani nchini Korea Kaskazini, amepelekwa hospitalini nchini Marekani.
Wazazi wa Otto Warmbier wanasema kuwa waliambiwa wiki iliyopita kuwa alikuwa hali mahututi.
Walisema kuwa walitaka ulimwengu ujue ni kwa njia gani wao na mtoio walivyohangaishwa na Korea Kaskazini,
Bwana Warmbier alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela na kazi ngumu, baada ya kukiri kuwa alijaribu kuiba bango lenye ujumbe wa propaganda.
Mamlaka za Korea Kaskazini zinasema kuwa alipewa tembe ya usingizi baada ya kuwa mgonjwa muda mfupi baada ya hukumu yake na tangu wakati huo hajaamka.
Watu wengine watatu raia wa Marekani bado wanaaminiwa kufunngwa nchini Korea Kaskazini.
0 comments:
Post a Comment